PATANISHO:Mke wangu aliniambia naweza endelea na maisha yangu baada ya kumchapa

Muhtasari
  • Mke wangu  amekuwa akija nyumbani kuchelewa ilhali hakuwa ametoka kazini
  • Nilipoenda kwake aliniambia niendelee na maisha yangu
Gidi na Ghost

Bwana Anthony Njoroge alituma ujumbe apatanishwe na mkewe Muthoni ambaye walikosana Oktoba mwaka huu baada ya yake kumchapa.

"Nilikosana mke wangu baada ya yake kuanza kuja nyumbani akiwa amechelewa, kuna siku alirudi nyumbani saa nne lakini hakuwa kazini

Nilipomuuliza alianza kuteta na nikamchapa alikusanya virago na akaenda kukaa pekeyake,nilipoenda kwake wiki jana na baba yangu aliniambia naweza endelea na maisha yangu

 

Hata hataki nione watoto wangu, kwa kweli napenda familia yangu." Alieleza Njoroge

Muthoni naye alikuwa na haya ya kusema,

"Kila kitu amesema ni ukweli, na hajazoea kunichapa nilimwambia anipe muda lakini niliona akiwa na haraka na kumwambia aendelee na maisha yake kwa maana aliniambia kuwa maisha yake yamesimama

Naomba anipe muda, na angoje jibu." Alisema Muthoni.