Mtu yeyote ana uwezo wa kua Rais - Ruto

Naibu rais William Ruto.
Naibu rais William Ruto.

Mtu yeyote  nchini anaweza kuwa rais. Naibu wa rais William Ruto anasema  urais haujawahi na kamwe hautakuwa akiba ya nasaba.

Alizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Mbunge wa Kabuchai James Lusweti.

Vile vile Ruto ametupilia mbali madai ya viongozi wa ODM kwamba kura ya maoni ya chaguzi tofauti itakuwa ngumu sana kwa wapiga kura.

Ruto amesisitiza kwamba Wakenya wamekua wakijaza  zaidi ya karatasi tano za kura katika uchaguzi mkuu na hawatapata shida kufanya hivyo katika kura ya maoni.

Hayo yakijiri, Taasisi ya Wahandisi imetoa wito kwa bosi wa NMS Mohammed Badi kuwazuia wasio wahandisi kuwasilisha miundo ya uhandisi kusaidia kukomesha kuanguka kwa majengo kwa sababu ya muundo duni wa muundo.

Baraza la magavana pia limeombwa kusaidia kaunti kukubali hatua hiyo na kuhakikisha ni wataalamu tu ambao wametimiza sheria ya uhandisi wanaoruhusiwa kuwasilisha ripoti za muundo ili idhiniwe.

 

Na tukivuka mipaka,Somalia inaishutumu Kenya kwa kuwapa silaha wanamgambo nchini humo kushambulia vikosi vyake mpakani  Mandera, siku chache baada ya kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na mshirika wake wa zamani.

Madai hayo ni ya hivi karibuni katika msururu wa shutuma ambazo Somalia imeitoa dhidi ya Kenya ikisema inaingilia mambo yake ya ndani.