Story za Ghost:Jamaa azuiwa kuingia baa kwa miezi 3 kwa kumpigia mwanamke magoti

Muhtasari
  • Jamaa azuiwa kuingia baa kwa miezi 3 kwa kumpigia mwanamke magoti
ghost
ghost
Image: RADIO JAMBO

Siku ya Jumatatu katika kitengo cha story za ghost alisimulia jinsi jamaa mmoja ametengwa na wenzake ambao wamekuwa wakibugia vileo nao.

Ni tabia na mienendo ambayo wengi hufanya na kutengwa na marafiki zao.

Je umewahi tengwa na marafiki zako kwa sababu ya jambo fulani, au kufanya kitu ambacho hakijawahi fanywa katika mtaa wenu?

Huu hapa usimulizi wake;

"Jamaa kiambu amezuiwa kuingia baa, na wala kubugia vileo na marafiki zake kaunti ya KIambu baada ya kumpigia mwanamke magoti

Alikuwa anampigia magoti amvishe pete ya uchumba, lakini marafiki zake walimwambia kwamba ni jambo ambalo halijawahi tendeka mtaa huo kwa hivyo kwa miezi 3 asiingie baa," Alisimulia.

Jamaa azuiwa kuingia baa kwa miezi 3. Sababu ikiwa, kumpigia mwanamke magoti. #StoryZaGhost #GidiNaGhostAsubuhi #OngeaUsikike

Posted by Radio Jambo on Sunday, August 22, 2021