Ni mambo ambayo tumekuwa tukiyaona kwenye filamu na kushangazwa sana, na kushindwa kama yanaweza kufanyika kwenye maisha ya sasa.
Ndio yanaweza kufanyika na hata kuwaacha wengi midomo wazi, katika kipindi cha toboa siri mwanamke mmoja amewapa wengi butwaa baada ya kumwaya mtama yale amekuwa akimfanyia shemeji yake.
"Nilibadilisha nambari ya simu na sauti ili kumjaribu shemeji yangu nione kama ni mwaminifu kwa dada yangu
ananijua kama Rukia kwenye nambari hiyo nyingine, kwani tumeoanga kupatana lakini nataka kumtobolea siri nimwambie kwamba ni mimi ambaye amekuwa akizungumza naye mitandaoni na kwenye simu yake,"Alieleza mwanadada huyo.
Yote tisa kumi ni kuwa alimfunga mumewe ili asiweze kutoa nje ya ndoa;
"MImi najua vyema mume wangu hawezi ni cheza kwani nilimfanyia mambo ili asinicheze, akinicheza tu kidogo atajua mimi ni mpokomo."
Huu hapa uhondo wote;