Deadbeat: Hashughulikii mtoto, hatungeoana kwa misingi ya kiukoo

Muhtasari

• Tina anasema alipata mimba na mwanamme ambaye baadaye alikuja kugundua ukoo haukubali kuoana na ikabidi wameachana.

• Mwanamme huyo alipopigiwa simu alimtaka Tina arudishe mtoto kwake kama yeye mwenyewe ameshindwa kumshughulikia.

Massawe Japanni
Image: Facebook

Tina anasema alipata mimba na mwanamme ambaye baadaye alikuja kugundua ukoo haukubali kuoana na ikabidi wameachana.

Alimuahidi atamsdaidia kulea mtoto lakini ikafika mahali jamaa huyo akacheza shere na kuacha kushughulikia malezi ya mwanae.

“Mtoto amefika grade 3 na huyo jamaa namwambia asaidie mtoto lakini anakataa kabisa,” Tina anaeleza.

Huyo jamaa ilifika mahali anamtukana na kumuambia kwamba amshugulikie mtoto mwenyewe Pamoja na yule mwanamme mwenye ameolewa na yeye.

Mwanamme huyo alipopigiwa simu alimtaka Tina arudishe mtoto kwake kama yeye mwenyewe ameshindwa kumshughulikia.

Lakini Tina anasema kwamba mtoto mwenyewe anakataa kuenda hata kukutana na babake.

Mwanamme huyo amesisitiza kwamba alikuwa anatumia mamake mpenzi wake ili kumsaidia mtoto kusoma lakini Tina amefutilia mbali madai hayo.

Tina anasema anachotaka huyo mwanamme ashughulikie mtoto ni karo ya shule na mambo mengine ya kuvaa na kula amuachie yeye atamudu.

Baada ya Tina kumwambia mwanamme huyo kwamba ako katika kituo cha kushughulikia maslahi ya watoto huko Kehancha, mwanamme huyo aliamuambia wakutane Jumatano ijayo ili wazungumze.

Mwanamme huyo amempa lawama Tina kwa kusema kwamba ana ujanja na ukora mwingi kwa sababu kuna wakati amewahi mdanganya kwamba mtoto amepotea na akasema hiyo ndio sababu kuu inayomfanya hawezi mtumia pesa kwa ajili ya malezi ya mtoto.

“Ninakwambia ukimpeleka mtoto shule, nipatie namba ya mwalimu mimi nitaongea na yeye na kumshughulikia mtoto lakini kukutumia wewe pesa, hapana. Wewe mpeleke mtoto shule lakini unipee namba ya mwalimu niongee na yeye kwamba mtoto asifukuzwe shule, niwajibike kama mzazi wake,” mwanamme huyo alisema

Je, unahisi nani mwenye makosa kati ya hawa wawili?