logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mwanadada azamia katika ulevi baada ya kugundua mumewe ana mpango wa kando

Alianza kunywa pombe katika juhudi za kupambana na msongo wa mawazo uliompata.

image
na SAMUEL MAINA

Vipindi15 February 2022 - 06:04

Muhtasari


  • •Evelyn alikiri kwamba alianza kunywa pombe katika juhudi za kupambana na msongo wa mawazo uliompata baada ya kugundua kuwa mume alikuwa anacheza ngoma nje ya ndoa.
  • •Alisema angependa waweze kuelewana na mumewe kwanza kabla ya kurudi kwa kuwa ni kawaida yake kugundua umuhimu wa mke wakati tu ako pweke.

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho mwanadada aliyejitambulisha kama Evelyn alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Daniel Kemboi ambaye walikosana mwezi jana kufuatia mzozo wa kinyumbani.

Evelyn alisimulia kuwa aligura ndoa yake ya miaka sita baada ya kupigwa vibaya na mumewe wakati alipogundua kuwa alikuwa amejitosa kwenye ulevi.

Alikiri kwamba alianza kunywa pombe katika juhudi za kupambana na msongo wa mawazo uliompata baada ya kugundua kuwa mume alikuwa anacheza ngoma nje ya ndoa.

"Nilipata mume wangu na mambo ya mpango wa kando. Nikijaribu kumueleza hakuwa ananielewa. Ilifika mahali nikawa na msongo wa mawazo nikaona nitumie pombe ili angalay niweze kulala vizuri. Sikujua nilikuwa naharibu maneno. Alipogundua nilikuwa natumia vileo, kuna wakati alinipiga usiku. Asubuhi ilipofika nilitoka nikaenda kwetu" Evelyn alisema.

Evelyn alieleza kwamba ingawa alikuwa amegura ndoa yake, bado kumekuwa na mawasiliano kati yake na mumewe na tayari amefanya juhudi za kumsihi arudi.

Alisema kuwa Kemboi alimhakikishia kwamba tayari amebadilika. Hata hivyo alisema angependa waweze kuelewana na mumewe kwanza kabla ya kurudi kwa kuwa ni kawaida yake kugundua umuhimu wa mke wakati tu ako pweke.

"Nataka tuelewane kwanza. Aliniuliza kama anaweza kutuma nauli nirudi nikamwambia asubiri jibu... Naumia sana na watoto. Nilipata ushauri kuhusu msongo wa mawazo. Hiyo ilinitoka, sasa niko sawa" Evelyn alisema

Juhudi za kuwapatanisha wawili hao hata hivyo ziligonga mwamba kwa kuwa Kemboi hakupatikana kwa simu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved