Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho, jamaa aliyejitambulisha kama Ben Omollo alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mkewe Loyce Makamu.
Omollo alisema mkewe ambaye wamekuwa pamoja naye kwa chini ya mwaka mmoja aliondoka tu bila kumpatia sababu yoyote na kurudi nyumbani kwao. Alifichua kwamba alimuoa Loyce akiwa na mtoto mmoja.
Omollo aliomba kusaidiwa kuwasiliana na mkewe ili afahamu kinachoendelea akidai kuwa hata hajakuwa akipokea simu zake. Alidai kwamba hakuwahi kumkosea mkewe kwa namna yoyote.
Loyce alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba hayupo tayari kumsamehe mumewe. Hata hivyo alisita kueleza sababu zake kugura ndoa yao.
Tazama jinsi Patanisho ilivyokuwa:-