Gidi amwambia Ghost si miongoni mwa waliochaguliwa mbinguni kulingana na Yesu wa Tongaren

"Mimi nimejihesabu kutoka Nairobi, huyu mwingine sijui," Gidi alisema.

Muhtasari

•Gidi alibainisha kuwa yeye ni miongoni mwa wachache waliochaguliwa kufika mbinguni siku ya kiama.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi, kitengo cha Story za Ghost, watangazaji Gidi na Ghost Mulee walimzungumzia mhubiri kutoka kaunti ya Bungoma kwa jina Yesu wa Tongaren na kauli yake kuhusu idadi ya Wakenya watakaofika mbinguni.

Kulingana na mchungaji huyo, watu wawili pekee kutoka kaunti ya Nairobi ndio wataenda mbinguni, huku watu wapatao elfu 168 kote duniani wakiwa ndio wateule pekee wa kufika katika Paradiso.

Gidi sasa amewaomba wakazi wa Tongaren kumpa maelezo zaidi kumhusu mhubiri huyo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa na jinsi anavyoendelea.

"Ikiwa unatoka tongaren na unajua yesu wa Tongaren ningependa kujua hali yake," alisema.

Wakati huo huo, mtangazaji huyo alibainisha kuwa yeye ni miongoni mwa wachache waliochaguliwa kufika mbinguni siku ya kiama.

"Mimi nimejihesabu kutoka Nairobi, huyu mwingine sijui," alisema.

Ghost hata hivyo alitilia shaka uwezekano wa mtangazaji huyo mwenzake kufika mbinguni.

Gidi pia alimweleza wazi mtangazaji mwenzake kwamba yeye si miongoni mwa wakazi wawili wa Nairobi waliochaguliwa kuenda Paradiso.

"Hauko kwa hiyo hesabu," Gidi alimwambia Ghost.

"Unajuaje?"  Ghost alimuuliza kwa kicheko.