logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mama mkwe alikuja nyumbani akamchukua mke wangu akisema ninamtesa

Hata hivyo, Daniel alikanusha kumtesa mke wake.

image
na Davis Ojiambo

Vipindi31 March 2023 - 06:19

Muhtasari


  • • Daniel alisema mke wake alimpigia simu hivi majuzi akimwambia kuwa hakuwa anamtesa na kumtaka kuhama ili arudi.
  • • Hata hivyo, mke alipigiwa simu na hakupatikana.
GHOST NA GIDI STUDIONI

Jamaa mmoja kwa jina Daniel kutoka kaunti ya Bungoma aliwasilisha ombi lake kwa Gidi na Ghost asubuhi ya Ijumaa akitaka kupatanishwa na mke wake Eunice.

Daniel alielezea kwamba mke wake alitoroka nyumbani pasi na kuwa na ugomvi wowote na alirudi kutoka kazini akapata mke hayuko nyumbani.

“Ilikuwa tarehe 20 mwezi huu nilitoka kazi nikapata mke ameondoka. Kupiga simu nyumbani mamake akashika na kuniambia kuwa alipata habari kwa majirani kuwa namtesa,” Daniel alisema.

Hata hivyo, yeye alishikilia kwamba hajawahi mtesa mke wake na Eunice alimpigia simu juzi akimwambia kwamba hakuwahi mkosea lakini akamtaka kufanya uamuzi wa kuhamia sehemu nyingine kama anamtaka arudi.

“Juzi ndio akanipigia akasema sijawahi mkosea akasema tutoke huko tuishi pahali tofauti. Yuko Bungoma kwao. Nataka tu aniambie ukweli kama atarudi ama hapana. Tumeonana tu mwaka jana,” Daniel alilia.

Hata hivyo, Gidi alimshuku Daniel kuwa huenda si mkweli, akihisi kwamba yake ni hadithi ya kubuni tu.

Watangazaji walipojaribu kumpigia Eunice, simu yake ilikosa kuingia, ikisema kwamba namba kama hiyo haipo katika matumizi kabisa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved