Mwanadada aliyejitambulisha kama Jemima Wanjiku ,29, kutoka Nakuru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Simon Waweru ,30, ambaye alikosana naye takriban miezi mitatu iliyopita.
Wanjiku alisema uhusiano wake na Waweru ulisambaratika mwezi Machi baada ya kumpigia simu kisha ikachukuliwa na mwanadada mwingine ambaye alimweleza kuwa ni mke wake halisi.
"Kuna wakati nilipiga simu ikiachukuliwa na msichana akaniambia ni bibi yake. Nilikuwa najua ni mpenzi wangu, hata tulikuwa tunapanga kuoana," Wanjiku alisema.
Aliongeza, "Nilikuwa na mimba yake. Kwa sababu ya stress, nikalazwa hospitali. Kumpigia simu akuje kuniona hakuja. Kakangu ndiye alikuja. Huwa tunaongea lakini sio sana. Saa zingine hachukui simu, saa zingine ananiblock. Saa zingine ananiambia ananipenda, mimi nimechanganyikiwa."
Wanjiku alisema alipomuuliza mchumba huyo wake kuhusu mwanadada aliyepokea simu yake alimweleza kuwa alikuwa anampima tu kuona kama anampenda.
"Sioni kama ako serious lakini nampenda. Nilikuwa nataka nijue msimamo wake. Sikuona kitu Aliniambia ako single eti hana bibi. Jana nilimpigia nikapata ameniblacklist. Kumpigia na simu ingine akaniambia atanipigia baadaye," alisema.
Mwanadada huyo alifichua kwamba hakuwahi kuishi pamoja na Waweru ila alikuwa amamtembelea mara kwa mara.
Waweru alipopigiwa simu alidai kwamba hamjui Wanjiku na kubainisha kuwa ako na familia kabla ya kukata simu.
"Huyu mimi simjui hata kidogo. Labda ni wrong number. Mimi niko na familia yangu. Ni wrong number," Wanjiku alisema.
Wanjiku alisema mchumba huyo wake hajawahi kuweka msimamo wake wazi kwani huwa anabadilika mara kwa mara.
"Haniambiangi msimamo wake ni upi. Wakati mwingine unapata ako na mood mbaya," alisema.
"Kutoka nitoke kwa ndoa nyingine sijawahi kupata mwanaume serious. Nilikuwa nimeona yeye ako serious. Nilikuwa natafuta mtu ako serious juu kukaa pekee yako ni ngumu," Wanjiku alilalamika.
Wanjiku alipopewa nafasi ya kuzungumza na Waweru hewani alisema, "Nakupenda sana. Nilikuwa natarajia tuoane kama bibi na bwana."
Je, uko na ushauri gani kwa Wanjiku?