logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa ampiga mkewe kufuatia hasira iliyochochewa na Chelsea kutoka sare na Arsenal

"Usiku ni shetani alikuwa amekuroga? Enda umuoe huyo shetani. Nitaenda kwetu nikae kama miaka miwili ndo nirudi," Kemunto alimfokea mumewe.

image
na SAMUEL MAINA

Vipindi31 October 2023 - 06:20

Muhtasari


  • •Lawrence alisema wasiwasi wake ulizidi usiku wa kuamkia leo kwani usiku kucha mke wake alikuwa akipanga virago na kuimba nyimbo za injili.
  • •"Usiku aliniambia niende nyumbani alete msichana mwingine. Mimi nikaamka. Ata niko kwa gari naenda," Kemunto alisema.
GHOST NA GIDI STUDIONI

Katika kitengo cha Patanisho, Lawrence Komenda (24) kutoka Kisii alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Yvonne Kemunto (20) ambaye alikosana naye takriban wiki mbili zilizopita kufuatia ugomvi wa nyumbani.

Lawrence alisema ingawa bado anaishi pamoja na mkewe, hakuna amani kabisa kwa nyumba kwani hata hawazungumzi.

"Tumekuwa tukikaa vizuri tangu nimuoe. Kukaakaa ikafika mwezi wa tisa tukaanza ugomvi, alinishuku niko na mipango ya kando. Juzi aliangalia akapata naongea na wasichana wa kanisa lakini ni juu mimi ni mwanachama wa kundi," Lawrence alisema.

Aliendelea, "Wakati wa mpira wa Chelsea na Arsenal nilienda kutazama, niliporudi nyumbani alichukua simu yangu tena akaangalia tena, mimi nikakasirika nikampiga. Saa hii ako kwa nyumba hatuongeleshani. Chakula anapika lakini akienda jikoni ni kuimba imba tu ata nikimuita hawezi kuitika . Anaimba tu nyimbo za injili."

Lawrence alisema wasiwasi wake ulizidi usiku wa kuamkia leo kwani usiku kucha mke wake alikuwa akipanga virago na kuimba nyimbo za injili.

"Hatuongeleshani. Amepanga vitu vyake. Usiku wote ni kuimba tu na kupanga vitu vyake, ni kama anataka kuondoka.Sikuwa na mpango wa kando ni kunishuku tu. Nilikuwa na yeye lakini tuliachana kitambo," alisema.

Aidha, alisema usiku ambao alimpiga mke wake alikuwa na hasira ambayo ilichangiwa na timu yake Chelsea kutoka sare na Arsenal.

"Hasira ya Chelsea kutoka sare na Arsenal ilifanya nikasirike nikampiga. Haongei, ni nyimbo tu kwa nyumba. Ni kumix nyimbo hata . Nikimuongelesha haongei . Chakula anapika vizuri, ananiwekea tu hakuli," alisema.

Kemunto alipopigiwa simu alisikika mwenye hasira tele na hata akaashiria wazi yuko tayari kuondoka na kumuacha mumewe.

"Mwambie aendelee kunikosea, sitaki aombe msamaha. Aombe msamaha kwa Mungu. Ata asikuje hapa leo, alale nje.  Mwambie tu akae mahali anataka. Acha tu nisimuabishe mbele ya watu," Kemunto alisema.

Aliendelea, "Usiku aliniambia niende nyumbani alete msichana mwingine. Mimi nikaamka. Ata niko kwa gari naenda. Si anataka kuleta huyo mwingine. Niko Mai Mahiu. Mwambie nimempikia chakula nimemuachia nyumbani."

Lawrence alijitetea, "Ilikuwa ni hasira tu. Rudi tukae pamoja. Nakupenda. Mimi simu yangu si huwa nakupea sijawahi kuficha. "

Kemunto alisema, "Usiku kwani ni shetani alikuwa amekuroga? Enda umuoe huyo shetani. Nitaenda kwetu nikae kama miaka miwili ndo nirudi. Utaleta huyo mwenye ulikuwa umesema utarudi."

Kemunto alimtaka mumewe kupunguza hasira zake iwapo wataendelea kuwa pamoja.

Lawrence alikubali kupunguza hasira na kumhakikishia mkewe kuhusu mapenzi yake mazito kwake.

"Mimi ata ni mtu wa choir pastor ananijua. Nakupenda, nitapunguza hiyo hasira," alisema Lawrence.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved