Peter Kamau ,33, kutoka Kayole alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Marieta Mutheu almaarufu Maggy ,28, ambaye alikosana naye mwaka jana.
Kamau alisema ndoa yake ya miaka miwili ilisambaratika wakati mkewe alipotoroka baada ya nyumba yake kufungwa kwa kutolipa kodi.
"Nilikuwa nimefunguwa nyumba. Nikaenda kazini alafu nikasuluhisha. Kurudi niliambiwa na landlord eti bibi amechukua nguo akaenda," Kamau alisimulia.
Aliongeza, "Nyumba ilifungwa siku ya Jumapili. Nikaambiwa na landlord niende nitafute pesa. Nilienda nikakosa. Jioni nikaambia landolord anifungulie juu ya mtoto. Kesho yake nikaenda kazini nikapata pesa na kulipa nyumba. Hatukuwa tumezozana naye. Nilikuwa nashuhughulikia mambo yote ya nyumbani."
Maggy alipopigiwa simu alilalamika kuhusu hatua ya mumewe kuhamisha vitu vyake bila idhini yake na akamuagiza azirejeshe.
"Sina mengi, cha kufanya ni jambo moja, huyo kijana anajua alichofanya. Alafu kuna vyombo vya nyumba, akiona vimemchokesha arejeshe nyumbani," Maggy alisema.
Aliongeza, "Nilikuwa nimenunua kila kitu kwa nyumba. Mimi mwenyewe alinipata nalipia nyumba, nikiwa nimenunua kiltu.. Alafu nisipate ameuza chochote. Arejeshe vitu vyangu alivyovipata kama anataka amani kwa hii dunia. Kila kitu kwa hiyo nyumba ni mimi nilikuwa namiliki. Huyo alikuwa mtu wa kusaidiwa. Vile zilikuwa nisipate ata moja haiko."
Kamau alijitetea akisema, "Nikipatana na huyu mwanadada nilikuwa naishi kwangu na yeye anaishi kwake. Alikuwa na deni ya miezi minne. Yeye ndiye alihamia kwangu na vitu zake zote. Mimi ndiye nilikuwa nalipa nyumba.
Hizo vitu anasema ni zenye alikuja nazo. Nilizipeleka Nakuru juu nilikuwa najenga huko. Nilimpigia simu akujie hakuwa anashika. Vitu zake ziko. Amesahau mimi ndiye nilimlipia ndio aruhusiwe kutoka."
Kuhusu kosa ambalo Maggy alidai alifanya hadi kupelekea wao kukosana, Kamau alidai kwamba mkewe alimfungia nje usiku kucha baada ya yeye kuenda matanga.
"Kulikuwa na matanga kwa jirani. Nikaalikwa na majirani. Kurudi ashafunga nyumba akiwa ndani. Nikamuomba afungue, akakataa. Nikakesha kwa stairs. Asubuhi nikaita landlord ambembeleze, akakubali," alisema.
Maggy aliendelea kusisitiza kwamba hawakuwa na uhusiano wowote na kumtaka arejeshe vitu zake.
"Hakuwa na idhini yangu. Hana haki kabisa. Simjui, alikuwa rafiki tu. Anaweza kurudisha vitu kwa caretaker ni rafiki yangu," alisema.
Aliongeza, "Hamna cha kurudiana. Saa hizi mimi simtambui kabisa. Hatukuwa tumeanza chochote. Alinipata na mtoto, sio wake. Alikuja kwangu nikamkaribisha. Usaidizi niliompa ni sawa, nitalipwa na Mungu."
Kamau hakuwa na budi ila kuheshimu msimamo wa mpenziwe.
Je, una maoni yepi kuhusu Patanisho ya leo?