logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa apigwa kalamu kwenye uwanja wa ndege kwa kutumia bangi, miraa

Bw Waweru alipopigiwa simu, Rabo alichukua fursa hiyo kumuomba msamana na kumsihi warejeshe uhusiano mzuri.

image
na SAMUEL MAINA

Vipindi07 June 2024 - 06:10

Muhtasari


  • •Rabo alisema uhusiano wake na rubani huyo wa ndege uliharibika Agosti mwaka jana baada ya yeye kufutwa kazi kwa kutumia mihadarati.
  • •Bw Waweru alipopigiwa simu, Rabo alichukua fursa hiyo kumuomba msamana na kumsihi warejeshe uhusiano mzuri.
GHOST NA GIDI STUDIONI

Jamaa ambaye alijitambulisha kama Silvester Rabo ,28, kutoka Busia alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na rafiki yake Captain Waweru.

Rabo alisema uhusiano wake na rubani huyo wa ndege uliharibika Agosti mwaka jana baada ya yeye kufutwa kazi kwa kutumia mihadarati.

"Kuna mahali nilikuwa nimeandikwa kazi alafu nikafukuzwa . Walisema hawatanipa mkataba mwingine. Nilikuwa naongea na Kapteni Waweru, akauliza nini ilifanya nifukuzwe. Nikamwambia nilichoambiwa. Baadaye akapatana na mtu mwingine akamwambia nilikuwa natumia mihadarati. Kuna wakati tulipatana na Kapteni akaniambia anajua nilifukuzwa juu ya mihadarati, yeye alichukua kama mimi ni muongo," Rabo alisimulia.

Aliongeza, "Singependa kukosana na huyo kapteni Waweru. Nilikuja kujua nilifukuzwa kwa sababu ya mihadarati. Nilikuwa natumia bangi, miraa na ile ya wahindi. Nilidhani wasiponiona hawawezi kujua. Ningetaka tuelewane na yeye kwa sababu ata haniongeleshi. Niliachana na mihadarati. Saa hii niko sober kwa mwaka moja unusu."

Bw Waweru alipopigiwa simu, Rabo alichukua fursa hiyo kumuomba msamana na kumsihi warejeshe uhusiano mzuri.

"Nathamini urafiki wetu na sitaki tuharibu uhusiano. Mimi nakuomba msamaha, kama utaweza naomba unisamehe," alisema Rabo.

Bw Waweru alikubali kumsamehe Rabo na kumwambia, "Usijali kaka yangu. Acha nikutafute. Sisi ni binadamu. Huwa tunafanya makosa. Bora unajifunza nayo, ndio muhimu."

Pia aliahidi kumtafuta kijana huyo na kuzungumza naye baadaye.

Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved