Binti anayejulikana kama Trizah Akoth,25 kutoka Mbita alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mamake,Hellen Adhiambo,57 baada ya kukosana miaka ishirini iliyopita.
Trizah alisema kuwa hajakuwa akiongea na mamake kwa takriban miaka ishirini.Mamake alikosana na babake na kuwaacha.Kwa sasa mamake yupo Oyugis.
"Baba alikuja akafariki nikiwa na miaka kumi.Tulikuwa wawili ,mimi na ndungu yangu mdogo.Tulikuwa tunaishi na nyanya na tulikuwa tunateseka sana.Nilienda nikaoleka nikiwa na miaka 19.Nilianza kufuatilia maisha ya mama,hadi nikapelekwa mahali alikuwa.Nilikuta ameendelea na maisha yake akiwa na watoto watano."
Aliongeza; "Nilipofika huko hakuwa ananijua,tulianza mazungumzo na akaanza kurejesha kumbukumbu pole pole na kuniambia kuwa alikuwa mamangu mzazi.Tulipokuwa tukiongea bwanake aliingia.Mama akaniambia kuwa wacha anisindikize ili nisimletee shida.Nikaamua kuenda ,baada ya miaka kidogo nilianza kuona shida,nikarudi kufuatilia tena.Nilipofika huko tena alinifukuza na kuniambia kuwa hanijui.Watu walijaribu kuniulizia nikawaambia kuwa huyo ni mamangu."
Akoth alidai kuwa watu wa hapo karibu walijaribu kumuuliza mamake ni kwa nini anamkana hasa baada ya mahojiano ya pande mbili.
"Alinikataa kabisa na mimi nilikisia kuwa huenda anaogopa ndoa yake itaharibika.Hata hivyo niliamua kurudi kwangu ,tulikalishwa chini na ndungu wake lakini bado alinikataa."
Akoth alisisitiza kujua ikiwa Hellen ni mamake mzazi wa kweli au la kwa kuwa kutokana na mambo aliyoonyeshwa yanamshtua.
Aliongeza kuwa ndungu yake mdogo alifariki;
"Ndungu yangu mdogo alifariki na nilipopeleka ripoti kwa mama hakuja.Nilitumana mtu,lakini mama aliponiona hakusongea hata karibu."
Mamake Trizah alipopigiwa simu ilipokelewa na jamaa ambaye hakujitambulisha akidai kuwa mamake Trizah hayupo.Alipigiwa kwa mara nyingine ila hakuna mtu aliyepokea.
Je,una ushauri gani kwa Trizah Akoth?