logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa alalamika mkewe kupigiwa simu, kuchat kitandani saa sita usiku

"Vile alifika kwao, ananipigia simu kudai pesa. Anasema kama siwezi kumtumia pesa nisimpigie simu," Evans alisema.

image
na SAMUEL MAINA

Vipindi18 July 2024 - 06:13

Muhtasari


  • •Evans alisema mahusiano yake ya takriban miezi sita yalisambaratika siku mbili zilizopita kufuatia suala la kutoaminiana.
  • "Vile alifika kwao, ananipigia simu kudai pesa. Anasema kama siwezi kumtumia pesa nisimpigie simu," Evans alisema.

Jamaa aliyejitambulisha kama Evans Mweresa ,27, kutoka Nyamira alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Olpah Muturi ,28, ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Evans alisema mahusiano yake ya takriban miezi sita yalisambaratika siku mbili zilizopita kufuatia suala la kutoaminiana.

Alidai kwamba mpenziwe amekuwa akizungumza na wanaume wengine mida ya usiku pamoja na kumkosea heshima kwa nyumba.

"Nilikuwa nampata na simu saa tano usiku. Nikimuuliza anazungumza na nani ananipigia kelele. Tukienda kwa kitanda, anafinya simu saa sita usiku. Nikimwambia afanye kitu anasema hakuja kufanya kazi alikuja kukaa," Evans alilalamika.

Aliendelea, 'Nilimwambia sitaki kumpiga aende kwao. Vile alifika kwao, ananipigia simu kudai pesa. Anasema kama siwezi kumtumia pesa nisimpigie simu. Nilimuoa akiwa na mtoto mmoja. Tulikuwa tunapanga tuende nyumbani kuchukua mtoto wake aje tukae. Sasa hivi akipiga simu nikose kushika, anatumia ya mamangu. Ananipigia simu anasema anataka kuenda kwetu. Hiyo ndo kitu inanisumbua."

Evans alisisitiza kujua msimamo wa mpenzi huyo wake na kudai kwamba hana nia ya kurudiana naye kwa sasa.

Hata hivyo, juhudi za kuwapatanisha wawili hivyo ziligonga mwamba kwani Bi Olpah hakushika simu zetu.

Evans alimalizia kwa kumwambia, "Kama umeenda ni sawa. Mimi nilikupenda na mtoto lakini ukaanza madharau."

Gidi alimshauri kutafuta mwanamke mwingine wa kuoa kwani mahusiano yake na Bi Olpah yalionekana kutofua dafu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved