Brian Muteithia ,26, kutoka Meru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Brenda Kananu ,20, ambaye mapema mwaka huu.
Muteithia alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilisambaratika Mei mwaka huu wakati ambapo mkewe aliondoka bila kueleza chochote.
"Hakuna kitu nilimfanyia hata kidogo. Aliamka tu akaenda. Nilikuwa nashughulikia kila kitu. Hachukui simu, akiona ni yangu anakata. Hajawahi kuniambia kitu. Alienda na mtoto," Muteithia alisema.
Brenda alipopigiwa simu, alifichua kwamba uamuzi wake wa kugura ndoa yake ulichochewa na mashemeji wake.
Alisema mashemeji zake walikuwa wakimtishia maisha na kuchukua vitu za nyumba, mambo ambayo yalimkosesha amani.
"Hakuna sababu, ni hivyo tu. Nilikosana na in-laws. Nilikosana na dada zake. Dadake mkubwa alikuwa ananitishia eti atanipiga, na imekuwa ni mazoea. Kuna wakati mwingine niliondoka na nikarudi," Brenda alisema.
Aliongeza, "Nilimwambia mume wangu lakini juu ako kazi mbali, ata akimwambia dadake aache, tukibaki nyumbani anaendelea. Nilikuwa nasoma chuo, nikirudi jioni nasumbuliwa. Niliona niende nyumbani nisome alafu nitarudi baadaye."
"Dada zake wanaingia mpaka kwa nyumba, wanachukua vitu. Wanasema ni nyumba ya kaka yao. Ni dada kama watano hapo, huwezi kufanya kitu"
Muteithia alimwambia mkewe, 'Urudi nyumbani nakupenda."
Brenda alisema, "Nitarudi nyumbani lakini sio sai, nitarudi nikimaliza shule. Sitaki stress, nimalize college. Nilikuwa natoka class, narudi. Nikirudi naenda nasumbuana nao kila wakati."
Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?