
JUKWAA la Songa Play linalotoa nafasi adimu kwa kila mtu kufurahia vipindi na miziki aipendayo nchini Kenya linazidi kuwavutia mashabiki wengi kutokana na maudhui ya kipekee nay a bila malipo.
Tangu kuzinduliwa kwa mara ya kwanza Agosti mwaka jana, Songa
Play limekuwa moja kati ya majukwaa machache ambayo yamejumuisha burudani la
kila aina kutoka kwa vipindi pendwa vya stesheni za Radio Afrika, Podikasti
zinazozungumzia mada mbalimbali hadi mikusanyiko na ngoma za kila aina.
Na katika kipindi hicho chote, baadhi ya maudhui na vipindi
ambavyo vimekuwa vikiwavutia wafuasi wengi ni pamoja na Toboa Siri ya Radio
Jambo.
Kipengele cha Toboa Siri ambacho hupeperushwa redioni na
Mbusii na Lion majira ya alasiri kimekuwa kikiwavutia wengi ambao hukifuata
kwenye Songa Play pindi wanapopitwa na wakati katika majira hayo ya jioni.
Katika Toboa Siri, watu hufungua roho zao kuelezea ya moyoni
ambayo mengine huwa ya kushangaza kwa jinsi yanavyosimuliwa.
Aghalabu, simulizi hizi huwa za matukio ambayo yanaweza
kumtokea mtu yeyote bila kujali tabaka lake maishani, hivyo kuwavutia watu
kutoka matabaka yote.
Kipindi kingine ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kama nembo ya
Radio Jambo na ambacho sasa kimevuta wimbo la ufuasi wake kwenye jukwaa la
Songa Play ni Patanisho.
Patanisho ni kipindi kinacholenga kuwapatanisha wawili ambao
wamekosana, kutokana na masuala ya kifamilia, mapenzi na urafiki.
Kipindi hiki pia huwapa watu nafasi ya kutoa maoni yao kwa
njia ya ushauri, kwani visa vingi vinavyoshughulikiwa kwenye Patanisho hutokea
katika maisha ya kila siku ya wengi wa Wakenya.
Songa Play pia imeshuhudia ongezeko la watu wanaojisajili kwa
ajili ya kufurahia mfululizo wa nyimbo zao pendwa ili kukata kiu yao kikamilifu
pasi na kusumbuliwa.
Miziki mbalimbali iliyoundwa kwa ajili ya wapenzi wa aina za
miziki kama Reggae, Rhumba, Gengetone, Arbantone, Bongo, Afrobeats, Amapiano miongoni
mwa nyingine imekuwa ikikosha nyoyo za mashabiki wengi wa Songa Play kwa muda
mrefu sasa.
Jambo zuri kuhusu Songa Play ni kwamba mtu halipishwi
chochote kujisajili ili kujipakulia burudani anayoipenda bila shruti.
Songa Play sasa inawajali hadi wale wanaotumia vifaa vya IOS
baada ya kuwa kwenye Android pekee katika siku za mwanzoni, kumaanisha kwamba
sasa kupata burudani kwenye jukwaa hili haijalishi kama unatumia Android ama
IOS, na, usisahau kujisajili ni bila malipo. Unangoja nini?...