Ilikuaje: Uhusiano kati yetu na mama wa kambo haujakuwa mzuri-Grace Ekirapa

Muhtasari
  • Mama yangu aliaga dunia tukiwa na umri wwa chini sana, hatukufurahia wakati mama wa kambo aliletwa kwetu
  • Nilikuwa nataka kuwa daktari lakini sikupita sana
  • Kuna wakati tulitamani mama yetu angekuwa hai, baada ya mama yangu kuaga tuliishi na shangazi wetu.
  • Niliumiza mtu roho ambaye hakustahili kuumizwa
  • Katika miaka minne yangu ya uhusiano wa kimapenzi aliyekuwa mpenzi wangu aliniacha mara tatu

Leo hii katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye mwanasaikolojia Grace Ekirapa ambaye alimpoteza mama yake akiwa na miaka nane huku akilelewa na baba yake mzazi.

"Kwetu tuko wasichana watatu, mama yangu alikuwa mgonjwa kila mara mwishowe akatuacha,baada ya miaka saba baba yangu alioa mke mwingine 

Ilikuwa ngumu sana kwa maana kila mtu huwa anatamani kulelewa na mama, baba yangu alikuwa anatulea kabla ya kuoa mke wa pili 

Tuliumizwa sana kwa maana tulikuwa tunajua mama yetu ameenda Mombasa baada ya yake kuaga dunia

Kuna wakati mimi na dada zangu tuliketi chini na kutamani mama yetu." Alizungumza Grace.

Ekirapa alisema kuwa alitaka kuwa daktari ilhali hakuweza kwa maana hakupita sana.

Huku akizungumzia uhusiano wake wa awali alisema haya,

"Niliachwa na aliyekuwa mpenzi wangu mara tatu katika miaka nne ya uchumba, aliniambia kuwa alikuwa anataka kuenda kuomba ili kuuliza Mungu kama mimi kweli ni wake

mara ya kwanza kuniacha nilikuwa hospitali baada ya kupata ajali, aliniambia kuwa hana amani kutuhusu

Baada ya hapo nilingoja mwaka mmoja, lakini sikufahamu kuwa ana mpenzi mwingine,baada ya kungoja alirejea na tukaanza uhusiano tena

 

Alienda tena na kurudi baada ya mwaka mmoja alienda na kisha akarudi na kusema ana hakika kuwa mimi ni mpenzi wake

Tulienda kwa wazazi miezi nne kabla ya harusi yetu alienda tena." Alieleza Grace.

Baada ya uhusiano huo kukamilika Grace alipata mwanamume mwingine na kubali uhusiano wake kwa maana alikuwa amekata tamaa.

Pia alisema kuwa mwanamume huyo alilipa mahari ilhali alimuacha na kumuumiza moyo.

Kwa mengi zaidi tembelea youtube ya Radiojambo kwa mengi zaidi.