Nilipoenda kumuona Sanaipei ili tufanye collabo ya wimbo wa 'wangu' nilimununulia Yoghurt-Nadia Mukami

Muhtasari
  • Nilitoa machozi baada ya wimbo wangu wa 'jipe kufanya vyema
  • Nilimbebea Sanaipei yoghurt nilipoenda kumuona ili tufanye collabo kwa wimbo wangu wa 'wangu'
Nadia Mukami

Leo hii katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye msanii Nadia Mukami ambaye amefahamika sana huku wimbo wake wa awali wa 'wangu' ukiwa umeenea sana kwenye mitandao ya kijamii.

"Nilipotoa wimbo wangu wa 'jipe' nilishtuka sana kwa maana corona iliripotiwa nchini ilhali nilikuwa nimetumia karibu nusu milioni na kila kitu kikasimamishwa, lakini wimbo huo ulifanya vyema sana 

Baada ya hapo nilitoa wimbo wangu wa 'wangu'ambao sasa umefanya vyema na kupata mapato mazuri

Nilipoenda kumuona Sanaipei ili tufanye collabo nilienda nikiwa nimembebea yoghurt alipenda sana wimbo wa wangu." Alisema Nadia.

Huku akizungumzia wimbo wake wa 'Jipe'alisema kwamba alimwaga machozi baada kuona wimbo huo unafanya vyema na kufikisha watazamaji milioni mbili licha ya kuwa na janga la corona na maeneo ya burudani yalikuwa yamefungwa.

"Nililia kwa maana kabla ya kutoa kibao hicho tulipitia changamoto nyingi na hata kutumia pesa nyingi sana

Kiini cha wimbo wangu wa 'Maombi' nilikuwa mtu mashuhuri lakini sikuwa na pesa, nilikuwa na shida na lebo ya rekodi yangu."

Nadia hakutembea peke yake studioni alikuwa naye Blessed Njugush ambaye yuko katika kikundi cha 'Jenga jirani initiative' ambapo wameamua kuwasaidia wanachi ambao wameathirika na janga la corona.

"Tumepanga kuwasaidia wanachi ambao wameathirika sana na janga la corona, ni hafla ambayo itakuwa tarehe saba na nane Novemba

Hata kama unataka kutusaidia unaweza tuma shillingi ata kama ni mia moja na tutashukuru." Njugush Alisema.