Nilimpoteza mume wangu miaka 16 iliyopita lakini naona ni kama jana-Mwanahabari Isabella

Muhtasari
  • Nilimpoteza mume wangu miaka 16 lakini naona ni kama jana
  • Nilipatana na mume wangu wa pili kila mmoja wetu akiwa katika hustle yake
  • Mume wangu aliaga dunia miezi mitatu baada ya kumzaa kifungua mimba wangu
Isabella Kituri

Leo hii katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye mwanahabari Isabella Kituri ambaye alisimulia safari yake uhanahabari na mambo mengine mengi.

Mwanahabari huyo ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto tano, huku akiwa katika  tasnia ya uhanahabari kwa miaka 18.

Huku akizungumzia kumpoteza mume wake alikuwa na haya ya kusema.

 

"Nilimpoteza mume wangu miaka 16 zilizopita, lakini kulingana nami naona ni siku moja, baada ya kumzaa mwanangu na kufikisha miezi mitatu mume wangu aliga dunia

nilipompoteza mume wangu nilikaa miezi miwili na kurudi kazini, mkubwa wangu alikuja nyumbani na kuniambia kukaa nyumbani sitapona na hakutanisaidia

Nilirudi nyumbani kwa wazazi wangu ambao walinisaidia kumlea mtoto wangu." Alieleza Isabella.

Mwanahabari huyo akizungumzia kuhusu nda yake ya sasa alisema kuwa mwanawe alimpokea baba yake wa kambo.

"Niliolewa tena na kubarikiwa na mtoto msichana, mwanangu alimkubali mume wangu na mume wangu amemkubali sana

Kwa hakika nina furaha katika maisha yangu na ninamshukuru Mungu, nilikaa miaka 14 ili niamue kuwa nataka kuwa katika mahusiano kwa maana ilikuwa inauma."

Mwanahabari huyo alisema kwamba anaweza kuwania kiti katika kaunti ya Taita Taveta majaliwa ya mwenyezi Mungu katika uchaguzi mkuu ujao 2022.

Kwa uhondo zadi tembelea Radiojambo youtube.