Kupoteza wanangu kulifanya nibadilike-Mkewe seneta Isaac Mwaura aeleza jinsi alipoteza wanawe

Muhtasari
  • Mkewe seneta mteuliwa Nelius Mukami alisema kwamba alijifungua mapacha watatu ilhali alirudi nyumbani na mtoto mmoja
  • Nelius pia alisema kwamba watu wengi walisema kwamba alimkubali mwanasiasa Mwaura kwa ajili ya pesa lakini si kweli

Hii leo studioni tulikuwa naye mkewe seneta mteuliwa Isaac Mwaura Nelius Mukami ambaye ni mwandishi, na baada ya kufunga ndoa alipitia changamoto tofauti.

Kulingana na Nelius alifanikiwa na mapacha watatu bali alitoka hospitali na mtoto mmoja baada ya wawili kuaga dunia.

"Nilizaa watoto wangu wakiwa na miezi sita, walipelekwa kwa wadi ya wagonjwa mahututi baada ya kujifungua nilikaa hospitalini kwa miezi mitatu

 

Baada ya kubarikiwa na mapacha watatu, nilitoka hospitali na mtoto mmoja kwa maana wawili waliaga dunia

Ni jambo ambalo lilifanya nipatwe na msongo wa mawazo kwa maana niliwatazama watoto wangu kwa miezi hiyo mitatu

Mwanangu ambaye hakuaga atafikisha miaka minne wiki ijayo, nikimtazama akikuwa kuna mambo ambayo amechelewa kufanya, pia amechelewa na kuongea

Huwa nawaambia watu wasilinganishe mwanangu na mtoto mwingine, kupitia hayo kulinifanya niandike zaidi." Alieleza Nelius.

Huku akieleza safari yake ya uandishi alisema kwamba alipewa motisha na mama yake ambaye alikuwa anawanunulia vitabu.

Huku akizungumzia ndoa yake na mumewe alikuwa na haya ya kusema.

"Simuoni mume wangu akiwa albino, kwa maana na muona akiwa mrembo sana, kuna baadhi ya watu walinikejeli na kusema kwamba niolewa na Mwaura kwa ajili ya ya pesa lakini si kweli." Alizungumza Nelius.

Kwa mengi zaidi tembelea chaneli cha radiojambo.