Mimi ni mwanadamu nilikuwa na hisia kwa Eric lakini simpendi-Carol BandBeca afichua haya

Muhtasari
  • Carol aeleza kuhusu uhusiano wake na Eric Omondi

Leo hii kwenye studio tulikuwa naye Carol Kamweru aliyezungumzia harusi yake na mchekeshaji Eric Omondi.

Carol alikuwa muigizaji katika kipindi cha Eric cha 'Wafe material'.

Akiwa kwenye mahojiano na radiojambo alikuwa na haya ya kusema.

 

"Ananipendeza lakini simpendi, katika kipindi cha wife material nilikuwa naigiza kulingana na kipindi lakini sifanyi hayo na kila kitu

mimi ni wanadamu, nilihisi kitu hisia huwa hazipotei tu hivyo lakini ninachosema simpendi Eric, busu ambayo tulipeana haikuwa katika kipindi lakini ilikuwa jambo nzuri." Alieleza Carol.

Pia alisema kwamba kuwa kwao katika kipindi hicho walitaka kusukuma albamu yao ambayo wametoa hivi majuzi.

Huku Becky akizungumza kumbusu Eric Omondi alisema kwamba hakumbusu kwa maana rafiki yake alikuwa tayari ameshaambusu.