Kama unajua wewe ni adui wa Ruth Matete jua wewe ni adui wa Mungu-Abel Amunga

Muhtasari
  • Abel Amunga azungumzia jinsi msanii Ruth alikejeliwa baada ya kumpoteza mumewe
  • Abel alisema kwamba Ruth hajawafika mahali pa kuwa wazimu kama vile baadhi ya wanaitandao wengi walisambaza habari
  • Faraja ya Ruth iko kwa mtoto wake sasa
Abel Amunga
Image: Radiojambo

Leo hii katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye muigizaji Abel Amunga ambaye pia ni baba yake msanii wa nyimbo za injili Ruth Matete.

Abel alizungumzia jinsi alimpoteza mkaza mwanawe yaaani mwendazake bwana yake Ruth Matete.

"Mambo mengi yalisemwa  kwenye mitandao ya kijamii baada ya kumpoteza bwana yake, maneno hayo yalitokana msimamizi mkubwa wa harusi yake wakati alirekodi Ruth na mumewe wakigombana wkati wa harusi

 

Baada ya Mkaza mwanangu kuaga dunia msimamizi huyo alipakia video hiyo kwenye mitandao ya kijamii na kisha lawama kuelekezewa na  mtoto wangu

Miezi miwili kabla ya mkaza mwanangu walikuwa wamefungua kanisa lakini alifunga na baadhi ya biashara zake ziliharibika kwa maana aliharibiwa jina

Ruth mahali alipoamesimama kwa ajili ya baadhi ya mashabiki ambao walisimama naye na watumishi wa Mungu

Faraja ya Ruth matete sasa iko kwenye mtoto wake, nataka kusema leo kama wewe ni adui wa Ruth Matete fahamu kuwa wewe ni adui  wa Mungu

Kuna wakati watu walitengeneza picha wakaeka kichwa cha Ruth kwa mwanamke mwingine na wakaanza kusema kwamba amekuwa wazimu nataka kusema Ruth hajawahi fika kiwango hicho

Mumewe alipoaga dunia ni mimi nilikuwa wa kwanza kujua kwa maana Ruth aliniita hospitali." Abel Alizungumza.

Abel alisema kwamba alimpoteza mke wake na kuwa hajaweza kuoa au kumpata mpenzi mwingine wa moyo wake.

 

"Ruth ana ndugu wengine wawili lakini wa kambo kwa maana baada ya mama yake kuniacha alienda kuolewa na kubarikiwa na watoto wawili."