Baba wa mtoto wangu aliniambia niavye mimba lakini nikakataa - Queen Lema

Muhtasari
  • Baba wa mtoto wangu aliniambia ni avye mimba lakini nikakataa Queen Lema aeleza jinsi amepambana na maisha
Queen Lema

Hii leo katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye video vixen Queen Lema ambaye ni mtanzania pia alieleza kwanini alichagua kazi ya video vixen, na magumu ambayo alipitia alipopata ujauzito.

"Nilikuja Kenya kwa ajili ya masomo, nilikuzwa na bibi yangu, wazazi wangu waliaga dunia nikiwa na miaka 8, ninlipmaliza kidato cha nne , nilijiunga na chuo kikuu cha Zetech

Nilidanganywa na mwanamume mmoja nikabeba ujauzito wake, nilipomwambia alikana akasema kwamba sio wake na ninapaswa kuavya mimba yenyewe

 

Nilikataa na kisha nikamzaa mtoto wangu, alimuona mwanangu siku moja tu kutoka ni mzae, nilimpelekea Nairobi hata hakumgusa alimuangalia na kuniambia, 'He is so tiny'

Baada ya tumeachana alipatwa na matatio kisha akajiua."Alieleza Queen.

Huku akieleza jinsi alipata kazi ya video visen alisema kwamba likuwa anaenda kazi usiku ya kudensi kisha asubuhi anafanya kazi ya keshia katika hoteli moja.

"Kuna rafiki yangu alikuja mahali nilipokuwa nafanya kazi ya keshia kwa hoteli akaniambia naweza kazi ya kudensi 

Nilikuwa naenda kudensi usiku mchana narudi kwa kazi yangu ya hoteli ili kuweka chakula mezani na kumlea mtoto wangu."

Queen aliweka mambo wazi kwamba aliacha kazi ya video vixen kwa ajili ya mwanawe.

"Niliamua kufanya jambo lingine mwaka huu, niliacha kazi ya video vixen kwa sababu ya mtoto wangu

Nimekuwa video vixen kwa nyimbo tatu."

Pia alisema kwamba amekumbana na wanaume ambao wanamwambia aende kwake wakafanye ngono usiku kucha kwa shillingi  milioni moja.