Mama yangu aliniambia kwamba ni mimi naharibu msanii Bahati-Msanii Vivian

Muhtasari
  • Vivian adai kwamba mama yake alimkashifu baada ya kushirikishwa katika kibao cha Bahati
Vivian

Katika kitengo cha ilikuaje tuikuwa naye msanii Vivian Wambui ambaye amefungua roho yake na kufichua mambo ambayo amekuwa akipitia au changamoto akipitia kwama msanii wa kike.

Vivian amekuwa akitoa kibao kimoja baada ya kingine huku vikipendwa na mashabiki.

Huku akizungumzia kibao chake na msanii Bahati alisema kwamba mama yake alimkashifu kwa sababu ya kutoa kibao hicho na msanii Bahati.

 

"mama yangu na baba yangu ni mashabiki wa muziki wangu, nilipotoa kibao na Bahati mama yangu aliniambia kwamba ni mimi namuharibu Bahati

Hii ni kwa sababu alikuwa anaimba nyimbo za injili, lakini sasa ni mimi namfunza kuimba secular, nilisema sawa." Alieleza Vivian.

Pia msanii huyo alisema kwamba amepanga kutoa albamu yake ya kwanza mwaka huu.

Kuna wakati ambao Msanii huyo alivuma sana kwenye mitandao baada ya kufichua kwamba anapitia magumu kwenye ndoa yake.

Akizungumzia swala hilo alisema kwamba,

"Kuna mahali tulikuwa tunatofautiana, kwa maana tulikuwa tu tunakuwa na tumelelewa katika mazingira tofauti, lakini tulienda kushauriwa na tukakua sawa."

Kwa mengi zaidi tembelea radiojambo youtube.