(+Video) Mimi nimetosheka na watoto sitaki kuzaa tena-Wahu Kagwi

Muhtasari
  • Msanii Nameless afichua kuna wakati alitoka kwake baada ya kukosana na Wahu
  • Wahu aisema kwamba hataki mtoto mwingine kwa sasa

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa na wanandoa Wahu Kagwi na Nameless ambao ni wasanii, na wanandoa wa kupigiw mfano na watu wengi.

Mapema wiki hii wasanii au wamevuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutoa kibao kipya kila mmoja wao kinachofahamika kama 'this love'.

Wawili hao wamebarikiwa na watoto wawili wa kike, huku Wahu akiongea alisema kwamba hataki kuongeza mtoto mwingine bali ametosheka na hao wawili.

 

"Mimi sitaki mtoto mwingine nimetosha wenye niko nao, lakini ninapo muonya mtoto mchanga najawa na furaha." Aliongea Wahu.

Pia wawili hao walifichua kwamba kuna wakati walikuwa na ugomvi wa nyumbani ambapo Nameless alibidi atoke kwa nyumba lakini walikuwa wanazungumza Wahu kupitia kwa simu.

"Mara ya kwanza tulikuwa na vita kwa maana hatukuwa tunajua mambo na ndoa, lakini kwa muda mnazoeana

Tukiwa tunachumbiana tulikuwa tunakosana alafu baada ya siku tatu tunarudiana, tumeachana kwa mara alafu natoka naenda lakii tunapigiana simu 

Naeza sema kutoka kwangu kwa nyumba baada ya kukeleleshana, kwa siku mbili au tatu tulikuwa tunachukua mapumziko kwanza," Alieleza Nameless.

Radio Jambo Kenya | Ongea Usikike | Ni kituo nambari moja Kenya kwa matangazo ya kiswahili. Vipindi vyake vina jumuisha Spoti,Mijadala moto moto na muziki wa Kiafrika #RadioJamboKenya Subscribe to RadioJambo Youtube - https://bit.ly/39wwc6u Mitandao ya Kijamii Instagram - https://rb.gy/e154d1 Facebook - https://rb.gy/09d1b9 Twitter - https://rb.gy/e23220

Wahu pia alisema kwamba

"Mtu unapaswa kuwa lazima ujukumikie furaha yako,sisi ni binadamu na kunawakati tunaweza angushana."