Nilimpa mama yangu mtoto wangu kiwa na miezi 13 baada ya kujifungulia jela-Beatrice Muriu

Muhtasari
  • Beatrice Muriu aelea maisha ambayo alippitia akiwa jela baada ya kufungwa akiwa na miaka 16
  • Alijifungulia jela huku akimpa mam yake mwanawe akiwa na miaka 13

Leo studioni tulikuwa naye Beatrice Muriu amabye alifungwa akiwa na miaka 16 na akiwa na ujauzito wa iezi nane.

Nini haswa kilichania kufungwa kwake hii hapa hadithi yake.

"Shida zilianza baada yangu kumaliza darasa la nane, nilikuwa na alama 406, niliitwa shule ambayo sikuwa nataka kuenda

 

Nilipofika kidto cha pili nilifukuzwa shule, nilifurahi sana, nilitoroka nyumbani, nikaenda kuishi na dadayangu, pia nilitoroka kwake nikaanza kuishi mitaani

KUna mwanamume ambaye alikuwa anakuja ananiuliza nafanya nini mitaani baada ya muda alinioa

Baada ya kupata ujauzito, ukiwa na miezi nane alitoka 'party' ilhali nilikuwa mgonjwa aliniitisha chakula lakini sikuwa nimepika kwa maana sikuwa najihisi vyema

Tulianza kupigana alinidunga visu kadhaa kwenye mkono wangu, naye nilimkata kwenye shingo, baada ya siku tatu aliaga dunia." Alieleza Beatrice.

Beatrice alisema kwamba baada ya mumewe kuaga dunia alikamatwa na kupelekwa katika jela ya wanawake ya Lang'ata.

"Baada ya wiki mbili nilipokuwa jela nilisikia uchungu wa kujifungua nilipelkwa hospitali ya Kenyatta nikaambia wakati wa kujifungua hujafika

Nilirudishwa jela, baada ya siku chache sikuhisi mtoto wangu akicheza nilienda kumwambia mama aliyefahamika kama Grace na kupelekwa hospitali ambapo nilifanyiwa upasuaji

Kwa ajili ya maisha ya jela si mazuri, nilimpigia mama yangu simu na akakuja kumchukua mtoto wangu akiwa na miezi kumi na tatu

Tayari mtoto wanu alikuwa amepatwa na ugonjwa wa kifua."

Beatrice alisema kwamba alimuambia mwanawe ukweli huku akisema kwamba anajuta kuwa mwanawe hatawahi muona baba yake halisi.

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo youtube