Nilifukuzwa nyumbani baada ya kubadili dini-Rose Muhando

Muhtasari
  • Rose MUhando aeleza jinsi alivyobadili dini huku akifukuzwa nyumbani kwao na kuishi mitaani
  • Pia aliweka mambowazi alikuwa na amani miezi tisa za kwanza kwenye tasnia ya burudani

Leo studioni tulikuwa na msanii wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Rose Muhando ambaye alizungumzia mambo kadha wa kadha.

Huku akieleza jinsi alibadili dini alikuwa na haya ya kusimulia;

"Nilipokuwa na miak saba nilipatwa na ugonjwa ambao haukuweza kutibiwa hospitalini, nilivimba kwenye kichwa changu

 

Usiku mmoja uifika nikakata tamaa nikamwambia baba yangu awache nikufe tu, usiku huo niliona mtu akiwa amevalia nguo nyeupe kisha akanishika mkono akaniambia ameniponya nismame nikamtumikie

Nilipuuza kwanza lakini nikiwa darasani hiyo sauti naisikia,nilienda kuwaambia wazazi wangu lakini hawakusikia niuliza mmoja wa  jirani yetu kwa akina yesu ni wapi 

Nilipoamua kumtumikia Mungu wazazi wangu walinifukuza, nikaenda kuishi mitaani

Nilipokuwa mitaani nilibarikiwa na watoto 3 ambao ninao sasa." Alieleza Rose Muhando.

Awali Rose amekuwa akivuma  kwenye vyombo vya habari kwa magumu ambayo amekuwa akipitia.

"Nilipoingia katika tasnia ya burudani nilikuwa na amani kwa miezi tisa za kwanza  lakini miaka hiyo nyingine sikuwa na amani

Nilichukuliwa kila kitu, mashamba,pesa na hata nyumba,ni jambo ambalo sitalizungumzia sana kwa maana ni la serikali."