Watu walinitenga baada ya kutoka katika lebo ya Otile Brown-msanii Jovial

Muhtasari
  • Msanii Jovial aeleza jinsi alitengwa na watu baada ya kutoka kwenye lebo ya Otile brown
  • Pia alisema kwamba ana uhusiano mwema na baba wa mtoto wake

Leo katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye msanii kutoka mkoa wa pwani Jovial ambaye aligusia mambo kadha wa kadha kuhusu kazi yake ya usanii.

Jovial alivuma wakati alitoka katika lebo ya msanii Otile Brown, huku akitengwa na marafiki zake.

"Nilipotoka katika lebo ya Otile brown licha ya yangu kufanya collabo naye watu wengi walinitenga na kuniambia kwamba nimeisha

 

Baada ya kurejea walianza kunisifu na hata kunipigia simu bali nilikuwa na wapa block,hivi karibuni mashabiki watarajie kibao kipya kutoka kwwangu na Otile

Huwa simpakii mtoto wangu kwenye mitandao ya kijamii, kwa maana sijui kama huwa au akikua atatka kuwa kwenye mitandao hiyo

Mimi na baba wa mtoto wangu huwa tunazungumza huwa anamsaidia mtoto wangu," Jovial Alizungumza.

Msanii huyo amekuwa akifanya collabo na wasanii tofauti humu nchini na hata kuvuma sana kwenye mitandao ya kijamii na hata nyimbo zake kupendwa na wanamitandao.