Naunga mkono ripoti ya mpango wa maridhiano BBI - Mwanasiasa Alinur akiri

Muhtasari
  • Mwanasiasa Alinur atangaza kuwania kiti cha ubunge Kamkunji
  • Pia alisema kwamba anaunga mkono BBI asilimia 100
Alinur
Image: Studio

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye mwanabiashara, mwanasiasa Alinur studioni ambaye alieleza safari yake ya kuwa mwanasiasa.

Alinur anafahamika kwa mazuri ambayo amekuwa akifanya katika jamii haswa kuwasaida wanyinge.

"Nilianza uongozi nikiwa darasa la sita, nilipoenda shule ya upili pia nilikuwa kiranja nilipoenda chuo kikuu pia nilikuwa kiongozi

Mwaka wa 2017 nilikuwa nataka kuwania kiti cha mwakilishi wadi wa Kamkunji lakini, kwa maana huwa tunapangwa na wazee Kamkunji waliniambia ningoje kidogo, nipata nafasi yangu mwaka wa 2022

Nikiwa kiongozi nataka kuwasaidia vijana, kwa maana wameumia sana katika jamii zetu,pia tunamtaka rais ambaye ni kijana kuanzi miaka 35 na kupanda

Naunga mkono BBI kwa maana ina mambo mazuri nilijiunga na siasa mwaka wa 2008," Alieleza Alinur.

Huku akizungumza ni kiti kipi ambacho atawania katika uchaguzi mkuu alisema kwamba,

"Nataka kuwania kiti cha ubunge eneo la Kamkunji mwaka wa 2022, mimi simpingi naibu rais na nampa heshima nyingi

Lakini wakati mwingine mafikira yake hayaendanishi na yangu,"