Kuna wakati Anwar alinitishia ataniua-Saumu Mbuvi afichua

Muhtasari
  • Saumu afunguka alichokuwa anapitia katika ndoa yake, huku akisema kwamba kuna wakati Anwar alimtishia maisha

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Saumu Mbuvi ambaye awali alivuma sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya kujitokeza na kufichua kile amekuwa akipitia katika ndoa yake.

"Nimekuwa na ugonjwa wa Bipolar kwa muda wa miaka nane sasa,kitu ambacho tulikuwa tunakosana na Anwar ni kwa sababu ya kulewa kwake

Wakati ambao nilijitokeza na kusema familia yang ilikuwa inapitia wakati mgumu, alikuwa ananichumbia kama rafiki ya baba yangu

 

Kitu moja ambacho naogopa katika maisha yangu sijui kukaa bila mchumba, kuna wakati alitumia vitu vyake na kisha akaja kunitishia kwamba ataniua," Alisema Saumu.

Huku akieleza jinsi walipopatana na Anwar alisema haya,

"Tulipatana kwenye mitandao ya kijamii ya facebook, kisha tukaanza kuzungumza, sijui kama anajua wala kufahamu mtoto anakula nini wala kula nini

Mimi namtakia maisha mema kwa maana si kitu kwangu, nina watoto wakulea, pia alinitumia jumbe akiniambia kuwa niko 'broke'

Sisi huwa tunasema ukweli," Alisema Saumu.

Saumu alisema kwamba kitu ambacho anaogopa sana katika maisha yake ni kutokuwa na pesa.

Kwa mengi zaidi tembelea radiojambo Youtube.