(+Video)Kujitegemea ni muhimu sana kama mwanamke-Susan Kaittany asema

Muhtasari
  • Mwanabiashara Susan Kaittany asema haya kuhusu wanawake

Leo katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Susan Kaittany, ambaye ni mkurugenzi mkuu kaika kampuni ya Posh palace.

Huku akiungumzia jinsi biashara yake imekuwa hasa wakati wa janga la corona mwaka jana alikuwa na haya ya kusema,

"Nadhani kila biashara  iliathirika wakati corona iliingia nchini, hatukuwa na wateja wengi kwa maana kila mtu alikuwa anaogopa virusi vya corona

Nilichojifunza mwaka jana ni kuwa kama mwanamke ni kitu kizuri kuwa na fedha zako na kijitegemea kama mwanamke ni vyema sana

Pia mwaka jana niligundua kwamba kuwekeza ni jambo njema, wakenya wengi hawawekezi lakini nadhani kila mtu alijifunza na corona," Alizungumza Susan.

Awali Susan alivumma sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukosana na Betty Kyallo huku akizungumzia jambo hilo alisema,

"Tulikuwa tumekosana kwa ajili ya biashara, lakini sitaongelelea jambo hilo sana, ukiwa kwenye biashara lazima upitie mambo mawili au matatu na lazima uvumilie kwa maana kuna changamoto nyingi," Alieleza.

Hii hapa video ya mahojiano hayo;

Radio Jambo Kenya | Ongea Usikike | Ni kituo nambari moja Kenya kwa matangazo ya kiswahili. Vipindi vyake vina jumuisha Spoti,Mijadala moto moto na muziki wa Kiafrika #RadioJamboKenya Subscribe to RadioJambo Youtube - https://bit.ly/39wwc6u Mitandao ya Kijamii Instagram - https://rb.gy/e154d1 Facebook - https://rb.gy/09d1b9 Twitter - https://rb.gy/e23220