King Kaka alitishiwa maisha baada ya kutoa kibao cha 'wajinga nyinyi'-Nana Owiti

Muhtasari
  • Mkewe King Kaka afichua haya baada ya kaka kutoa kibao chake cha 'Wajinga nyinyi'

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye mkewe rappa King Kaka Nana Owiti, huku akizungumzia kibao cha King Kaka alichotoa na kuvuma sana alisema kwamba msanii huyo alipokea vitisho vingi sana.

Pia alisema wakati huo Desemba hawakusheherekea wala kuenda kujivinjari kwa maana walikuwa wanaogopa sana.

"Sikujua akitoa kibao hicho, niliamka asubuhi  nikapata nimepigiwa simu nyingi sana, kwanza mama alinipigia simu na kuniuliza kwanini nilikubali bwana yangu atoe kibao kama hicho

 

Baada ya kibao hicho King aka alitishiwa maisha sana, ata nakumbuka hatukusheherekea sikukuu ya krismasi kwa sababu tulikuwa tunaogopa sana

Kuna mtu ambaye alitupigia simu na kutuambia kwamba Kaka anahitajika na DCI, lakini kabla ya kuenda aandike kwenye mitandao a kijamii ya twitter kama kiu chochote kitatokea

Tulipofika kwa DCI walituambiwa kwamba hawakumuita hapo, naweza sema Kaka alijivunia kutoa kibao hicho kwa maana alifungua watu wengi macho na kuongelelea watu ambao hawangeongea lakini walikuwa wanajua ukweli," Nana Alieleza.

Nana akizungumzia maisha ya utoto wake alisema kwamba alimpoteza mama yake akiwa na miaka 19.

'Mama yangu alinizaa akiwa shule ya upili, kisha akarudi shule, baba yangu aliaga dunia nikiwa darasa la tano

Sikuwa na uhusiano wa karibu na baba yangu wa kambo kwa sababu alikuwa mtu wa kusafiri alikuwa rubani

Mimi nimekula shida, ndio maana napenda  kutia bidii katika kazi yangu napenda pesa zangu sana

 

Nilipatana na Kakak kwa barabara, nilikuwa naenda kununua marashi, na yeye alikuwa na biashara yake hapo

Nilimsalimia na kisha tukaanza kuongeleshana, ukweli ni yeye aliniita nana kwa sababu naitwa nini,"