Nilifahamu Amber Ray ni mke mwenza wangu kupitia mitandaoni-Mkewe Jamal aweka mambo wazi

Muhtasari
  • Mkewe Jamal Roho safi aweka mambo wazi kuhusu Amber Ray
Image: Studio

Katika kitengo cha ilikuaje, tulikuwa naye mkewe Jamal Rohosafi Amira ambaye aliweka mambo wazi kwamba alifahamu Amber Ray ni mke mwenza wake kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

Akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba hawatakuwa sawa na Amber Ray.

PIa alisema kwamba hakufahamishwa na mumewe kuhusu Amber Ray,ingawa ni sawa kwa waislamu kuoa bibi wa pili Amira alisema kwamba jambo hilo halikufanywa kwa njia inayofaa.

"Ukweli ni kwamba sikufahamishwa wala kujulishwa,lilifanya mambo yawe mabaya zaidi, nilijua kuwa Amber Ray ni mke mwenza wangu kupitia kwenye mitandao ya kijamii, kama mama hata wewe unajua vile utasikia," Alisema Amira.

Amira aliongeza na kusema haijakuwa jambo la rahisi na halitawahi kuwa na hatawahi ongea na Amber.

"Huwa siongei naye na sitawahi kuwa rafiki yake, ni jambo ngumu kwangu na kama mama ungesikia vile vile

Haijawahi kuwa rahisi kwangu na haitawahi kuwa, natamai nitauwa sawa, niko sawa na nina furaha na yale nafanya,"