Mume wangu aliwaambia watoto wangu kuwa mimi ni mwendawazimu-Virginia

Muhtasari
  • Virginia asimulia jinsi alipitia mateso mikononi mwa mumewe
Virginia Wangari
Image: Studio

Leo hii katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Virginia Wangari ambaye ni mama wa watoto 12, alisimulia mateso ambayo alipitia akiwa mikononi mwa mumewe.

Licha ya mumewe kuwa muhubiri mkubwa katika dini ya wakorino, alitoa utabiri na kusema kwamba Mungu amesema hapaswi kuwa na wanawe.

Wakati huo mwanamwe wa kumi na 11 alikuwa na miezi mitatu, huku akifungiwa kwenye chumba akiwa pekeyake, na mume kuwaambia wanawe kwamba mama yao amekuwa mwendawazimu.

"Baada ya kujifungua mtoto wangu wa 11, akiwa na miezi mitatu, mume wangu ambaye alikuwa ni muhubiri katika kanisa la wakorino alitabiri na kusema kwamba Mungu amemwambia sistahili kuwa naye na kuwa sikusikia uchungu wa watoto wangu

Alinifungia kwa nyumba kwa miezi 3 na akawaambia watoto wangu kuwa mimi ni mwendawazimu, nikiwa katika kile chumba alikuwa anakuja na kunitesa na hata kunibaka, mtoto wangu wa kumi na 12 ilikuwa wakati alinibaka," Alieleza Virginia.

Wahenga hawakukosea waliposema kikulacho ki kunguoni mwako,Virginia alisema kwamba rafiki yake wa karibu ndiye alikuwa mke wa mume wake.

"Baada ya kuachana na mume wangu rafiki yangu wa karibu ndiye aliweza kuolewa na mume wangu, alikuwa ananitumia jumbe mbaya, na hata waliwatesa watoto wangu,"

Kwa mengi zaidi tembelea mitandao ya kijamii ya Radiojambo youtube.