Mama yangu aliaga dunia nikiwa jela ilikuwa uchungu-Grace Akinyi afichua

Muhtasari
  • Kwa nini mhadhiri Grace Akinyi alifungwa jela? soma uhondo wote
  • Mumewe alikuwa anaenda kumtembelea lakini hakuwa anajitambulisha kama mumewe
Grace Akinyi
Image: Studio

Leo katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye Grace Akinyi ambaye alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu lakini ailifika wakati akakamatwa.

Sababu ya kufungwa jela ni ipi? huu hapa usimulizi wake;

"Nilikuwa nimeolewa, baada ya kubarikiwa na watoto 4 mume wangu alianza kuenda nje ya ndoa tukaachana

Kwa sababu nilikuwa na watoto nilihitaji pesa, nilipata mradi wa kuenda pakistan, nilichukua mkopo ili nifanye biashara hiyo, kwa kweli sikuelewa ni biashara ipi

Nilipofika pakistan, nilipewa dawa za kulevya kuja kuuza kenya,nilikamatwa  nikiwa kwenye uwanja wa ndege na nikafungwa

Sikumtaja mama mwenye bashara hiyo, lakini niliwaambiwa polisi kila kitu kwa maana nilikuwa nimeshtuka

Baada ya muda alikamatwa na kushtakiwa na kupatwa na hatia," Alieleza Grace.

Mumewe alikuwa anaenda kumtembelea lakini hakuwa anajitambulisha kama mumewe.

"Mume wangu alikuwa anakuja kunitembelea jela, ananiletea pesa lakini, alikuwa anaitabulisha kama ndugu yangu kwa maana alikuwa aktari hakuwa anataka kuharibu sifa za mahali pa kazi

Pia nilikuwa nimeingia kwenye biashara hiyo kwa maana nilihitaji pesa za matibabu ya mama yangu

Mwaka mmoja kabla ya kutoka jela, nililetewa habari mbaya zaidi kwamba mama yangu ameaga dunia ilikuwa uchungu

Najuta sikumwambia mama yangu yakle nilikuwa napitia katika ndoa yangu, kwa maana ningemwambia singepitia hayo yote,"

Kwa mengi zaidi tembelea radiojambo youtube.