Nilipigwa risasi tisa,sijawahi pata haki-Richard asimulia

Muhtasari
  • Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Richard Muema ambaye alipigwa risasi tisa mwaka wa 2019 na wezi katika eneo la Kasarani
Massawe Japanni
Image: Studio

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Richard Muema ambaye alipigwa risasi tisa mwaka wa 2019 na wezi katika eneo la Kasarani.

"Ilikuwa saa nne ya usiku ambapo nilikuwa nimeenda kuweka pesa kwa simu niikuwa na rafiki yangu ambaye tulikuwa tumetoka kula naye,

Wezi hao walikuwa wametungoja nche, tulikaa sana waliona hatutoki waliingia kwenye duka, mmoja wao alimpiga rafiki yangu risasi kwenye mabega

Mimi nilipigwa risasi saba tumboni,mguu moja na mkono moja, ya mkoni haikutolewa nimekuwa nikitembea nayo," Alieleza.

KUlingana na Richard ata baada ya kisa hicho kutekea hajawahi pata haki yoyote, bali ana mke ambaye ni mzuri kwani amekuwa akimsaidia baada ya hayo yote.

Baada ya kisa hicho Richard aliwekwa mfuko wa kuendea haja kubwa,ambayo akienda kutolewa mara tatu kwa wiki anahitaji shillingi 1500.