'Sikuwahi kuwa na urafiki nao' Mavoko azungumzia uhusiano na Diamond & Harmonize

Mavoko ambaye alijitoa Wasafi miaka mitatu iliyopita amesema kuwa hajawahi kutana na wawili hao tangu agure Wasafi.

Muhtasari

•Staa wa Bongo Rich Mavoko amekiri kuwa hajawahi  kuwa na urafiki na bosi wa Wasafi Diamond Platinumz wala Harmonize.

•Akizungumza na Massawe Japanni kwenye kitengo cha 'Ilikuaje?', Mavoko alieleza kuwa uhusiano wake na waliokuwa nao Wasafi ulikuwa wa kibiashara tu ila hawakuwa marafiki.

Image: INSTAGRAM

Staa wa Bongo Rich Mavoko amekiri kuwa hajawahi  kuwa na urafiki na bosi wa Wasafi Diamond Platinumz wala Harmonize.

Mavoko ambaye alijitoa Wasafi miaka mitatu iliyopita amesema kuwa hajawahi kutana na wawili hao tangu agure Wasafi.

Akizungumza na Massawe Japanni kwenye kitengo cha 'Ilikuaje?', Mavoko alieleza kuwa uhusiano wake na waliokuwa nao Wasafi ulikuwa wa kibiashara tu ila hawakuwa marafiki.

"Hatujawahi kutana naye(Diamond".. mimi niko sawa. Wote tuko nao sawa ila hatujawahi kutana nao (Diamond na Harmonize). Inabidi watu watofautishe urafiki na biashara, sikuwahi kuwa rafiki na hao watu, nilikuwa nafanya biashara pale. Kabla hata niende Wasafi, nilikuwa nafanya muziki pekee yangu. Sikuwahi kuwa na urafiki na Diamond , aliponihitaji tufanye kitu pamoja, mimi nilifanya kama biashara sio urafiki" Mavoko alisema

Alipoulizwa sababu zilizompelekea kuondoka Wasafi, mwanamuziki huyo alitaja kuwa kulikuwa na tofauti za kibiashara ila akasita kufafanua zaidi kuhusu mzozo ambao uliibuka. Alisema kuwa alitaka kufanya muziki wake kama alivyotaka mwenyewe.

"Watu wanahitaji kuelewa kuwa ile ni biashara. Ikifika kipindi nione nataka kufanya biashara yangu vile ninavyotaka na  naona nashindana na wewe hamna haja ya kugombana ninaweza kuondoka. Ni biashara tu hamna kitu kibaya" Alisema Mavoko

Mavoko alisema kuwa hakuna utofauti wowote ambao ulitokea baada yake kuondoka pale