Familia yangu ilinizika ilhali niko hai-Jamaa atoboa siri

Muhtasari
  • Familia yangu ilinizika ilhali niko hai-Jamaa atoboa siri
  • Katika kitengo cha toboa siri jamaa mmoja alitoboa siri jinsi alizikwa na familia yake ilhali yuko hai
  • Hayo yalitendeka mwaka wa 2019, nilikatwa mkono lakini mama huyo alinipeleka hospitali
Mbusi na Lion

Katika kitengo cha toboa siri jamaa mmoja alitoboa siri jinsi alizikwa na familia yake ilhali yuko hai.

Je nini kilisababisha mazishi yake? 

Huu hapa usimulizi wake

"Nilitoka nyumbani ni kakuja Nairobi kutafuta kazi, nilipata kazi ya wizi, wakati mmoja tulienda kuiba na marafiki zangu lakini tulipokezewa kichapo

Watu walidhani nimeaga dunia, lakini nilikimbia nikaenda kusaidiwa na mama ambaye anafahamika kama mama Muthoni

Familia iliambiwa kwamba nilifanya ajali nikiwa kazini, walienda kwenye makafani ya kuhifadhi maiti walimpata mtu alikuwa anafanana na mimi na wakaenda kunizika

Walinizika na kuniwekea msalaba mkubwa sana kwenye kaburi langu, niliona kwa picha za marafiki zangu

Hayo yalitendeka mwaka wa 2019, nilikatwa mkono lakini mama huyo alinipeleka hospitali sasa namfanyia kazi

Nataka kutobolea familia yangu siri, na kuwaambia kwamba niko hai, lakini nashindwa jinsi nitarudi nyumbani," Alitoboa siri mwanamume huyo.

Je ushauri wako kama mwanajambo ni upi?