Mwajiri wangu aliniambia sijui kuosha sehemu zangu za siri baada ya kunidhulumu kingono-Topister

Muhtasari
  • Topister aeleza alivyopitia mateso mikononi mwa mwajiri wake
Topister
Image: Studio

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye Topister, ambaye alipitia changamoto nyingi alipokuwa na umri mdogo.

Kulingana na Topister alianza kufanya kazi ya nyumba alipokuwa darasa la tatu, kwa sababu ya changamoto nyingi za maisha.

Huku akieleza hadithi yake alisema kwamba baada ya kuajiriwa mwajiri wake alimdhulumi kingono, lakini alipomwambia mkewe alimkemea na kumlaumu.

"Jamaa mwenye nyumba aliniambia ananitaka, nikaja nikamwambia mama mwenye nyumba ila akaniambia kwamba ni kama nimetumwa nije kuharibu ndoa yake.

Akaniambia nilale niote tena akisema hakuna vile mumewe angetaka mtoto kama mimi ambaye hajui kuoga.

Nilikuwa ninakaa na bibi. Shangazi yangu ndiye alikuwa anatusaidia na kwa bahati mbaya akaaga dunia.

Ikabidi niache shule maanake bibi hangeweza... Nilianza kufanya kazi 2003 nikiwa na miaka 15... Sikuwa ninalipwa, pesa ilikuwa inatumiwa mama.

Mumewe alifanya tendo la ndoa na mimi nikiwa nimesima akasema nikipiga nduru hatanipeleka hospitalini maanake nilikuwa nimevunjika mkono.

Sikuwa hata ninataka mkewe aende dukani maanake hapo ndio alikuwa anapata nafasi ya kufanya mapenzi nami,baada ya tendo la ndoa aliniambia kwaba sijui kuosha sehemu zangu za siri," Alieleza Topister.

Alzidi na kuelezea hadithi yake na kusema kuwa;

"Nilipotoka kwa hiyo nyumba, nilipatana na mpenzi akanipa ujauzito kisha akaniruka. Nikapata mtoto ila akaja akaaga dunia baadaye. Nilijifungua nikiwa na miaka 16

Baba yangu alikanyaga kaburi la mtoto wangu, nikaskia kuwa sitawahi jifungua tena kwa maana baba yangu alifanya kitendo hicho

Nilifurai sana nikamshukuru Mungu nikawambia kama hiyo ndio 'Family planning' amenipa nimefurahi,"

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.