Nilisimamishwa kazi kwa kufichua kwamba nadhulumiwa na wakubwa wangu-

Muhtasari
  • Viviana afichua kwanini alisimamishwa kazi kama polisi
Viviana HYline
Image: Studio

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Viviana Hyline. Alikuwa afisa wa polisi. Wiki chache zilizopita, alirekodi video akidai kwamba amekuwa alidhulumiwa na wakubwa wake bila kupata haki.

Juhudi za kutuma barua za kijiuzulu ziliambulia patupu.

Akiwa kwenye mahojiano, alisema kwamba ana msongo wa mawzo baada ya kusimamishwa kazi.

"Nimekuwa mgonjwa kwa  muda, sikuwa nalala nikiwa kazini, sababu yangu kuu ya kufanya kazi kwa msaa mingi, mkubwa wangu alinitongoza lakini na nika mkataa hapo ndio shida zangu zilianzia 

Alikuwa ananifanyisha kazi kwa masaa nyingi kuliko kawaida, nilikuwa nakunywa dawa ili niweze kulala lakini sikuwa na lala

Niliamua kutumia video hiyo kueleza masiabu yangu, kwa maana polisi wanawake wanapitia mambo mengi lakini wanyamaza wakiogopa kunyanyaswa

Nilisimamishwa kazi kwa ajili ya kufichua kuwa nimekuwa nikidhulumiwa na wakubwa wangu," Alondea Viviana.

KUlingana na Viviana,polisi wanawake wamekuwa wakipokea dhuluma nyingi, na kusema kwamba katika sekta ya polisi kuna ufisadi.

"Sisi tunafanya ufisdi mwingi sana kwa sababu ukitaka kuhama mahali pa kufanya kazi lazima ununue kuhama kwako au nafasi yako, wanawake pia wamekuwa wakipokea dhuluma kutoka kwa wakubwa wao."

Pia alisema kwamba marafiki zake walimtenga baada ya kupakia video hiyo mitandaoni, huku baadhi yao wakimtishia na kumwambia kwamba maisha yake yamo hatarini baada ya kuwataja wakubwa wake majina.

wa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.