'Usimdhihaki Mungu,'Janet Otieno awajibu wasanii waliokashifu tasnia ya nyimbo za injili

Muhtasari
  • Janet Otieno awajibu wasanii waliokashifu tasnia ya nyimbo za injili
janet.otieno
janet.otieno

Kwa muda sasa tumeshuhudia na kuona tasnia ya nyimbo za injili ikipewa kejeli nyinhi na kukashifiwa na baadhi ya wasanii ambao walikuwa wakiimba nyimbo za injili.

Wiki chache baadhi ya wasanii wamesema kwamba watu walio kwenye tasnia ya nyimbo za injili ni 'shit' na wala sio tasnia ambayo ni mbaya.

Msanii wa nyimbo za injii Janet Otieno akiwa kwenye mahojiano na Radiojambo aliwajibu na kuwashambulia wasanii ambao wanakashifu tasnia ya nyimbo za injili.

Kulingana na Janet wasanii hao hawapaswi kumdhihaki Mungu wala kuhukumu wasanii wenzao.

"Kile wasanii ambao wanakashifu tasnia ya nyimbo za injili wanapaswa kufahamu hawapaswi kuhukumu, pia wasimdhihaki Mungu

Wanapozungumza mabaya kuhusu tasnia ya nyimbo za injili sisi wasanii wa nyimbo za injili ttupo pale tunanyamaza, ukisema wasanii walio kwenye tasnia ya nyimbo za injili ni 'shit' ata wewe jione na kuacha kuhukumu

Kwa muda sasa wasanii wamekuwa wakikashifu tasnia ya nyimbo za injili na sio vyema," Janet alisema.

Siku chache zizlizopita Janet amezindua kibao kinacho fahamika kama Siri.

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.