Jacky Vike afichua kilichomfanya arudiane na mpenzi aliyemcheza na rafikiye wa karibu

Muhtasari

•Mama huyo wa mtoto mmoja aliweka wazi kwamba katika maisha yake yote amewahi kuwa kwenye mahusiano matatu tu.

•Licha ya mpenzi wake kutokuwa mwaminifu, Jacky bado alirudiana naye kwa kuwa alihisi kama kwamba hakuwa na kwa kuenda.

Jacky Vicky katika mahojiano na Massawe Japanni
Jacky Vicky katika mahojiano na Massawe Japanni

Mgeni wetu leo katika kipindi cha Bustani la Massawe, Kitengo cha Ilikuaje alikuwa mwigizaji Jacky Vike almaarufu kama Awinja kutokana na nafasi aliyoigiza katika kipindi cha Papa Shirandula.

Jacky alifunguka kuhusu masuala mbalimbali ya maisha yake ikiwemo familia na mahusiano yake.

Mama huyo wa mtoto mmoja aliweka wazi kwamba katika maisha yake yote amewahi kuwa kwenye mahusiano matatu tu.

"Nimechumbia wanaume watatu tu. Kwa kweli nahitaji kujaribu zaidi" Jacky alisema.

Mwigizaji huyo alikiri kwamba amewahi kuwa kwenye mahusiano sumu ambapo mpenzi wake alirusha roho na rafikiye wa karibu.

Licha ya mpenzi wake kutokuwa mwaminifu, Jacky bado alirudiana naye kwa kuwa alihisi kama kwamba hakuwa na kwa kuenda.

"Alikuwa amepunguza kujiheshimu kwangu. Nilihisi sikuwa mzuri kutosha. Aliniweka mahali ambapo singeweza kutoka. Alikuwa amezima nyota yangu" Jacky alisema.

Mwigizaji huyo ambaye alicheza nafasi ya kijakazi katika boma ya Papa Shirandula alisema kwamba mpenzi wake alimcheza na mmoja wa maafiki wake wa karibu ambaye aliyaminia sana.

Jacky aliweka wazi kwamba jamaa aliyemtendea hayo sio baba ya mtoto wake. 

"Ilichukua muda kwa moyo wangu kupona. Nashauri watu wajue dhamani yao. Mtu asiwahi kufanya kama wewe sio kitu. Usikubali kukaa mahali ambapo huna amani ama unahisi hupendwi" Jacky alisema.

Alifichua kuwa kwa sasa ako kwenye mahusiano na  mpenzi mwingine. Alisisitiza kwamba hana mpango wa kupata mtoto mwingine hivi karibuni.