Jay Melody afichua wasanii Wakenya anaowashabikia sana

Mwimbaji huyo wa kibao 'Sugar' alikiri kuwa mwanzoni alikabiliwa na changamoto kubwa

Muhtasari
  • Melody aliweka wazi kwamba taaluma yake ya muziki ilingo'a nanga vizuri takriban miaka sita iliyopita baada ya kuwachia kibao 'Goroka'
Image: INSTAGTAM// JAY MELODY

Studioni katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa naye msanii maarufu kutoka Tanzania Jay Melody ambaye amezungumzia safari yake ya usanii.

Melody aliweka wazi kwamba taaluma yake ya muziki ilingo'a nanga vizuri takriban miaka sita iliyopita baada ya kuwachia kibao 'Goroka'

Pia alidokeza kuwa alikabiliwa na tatizo la kukataliwa na baadhi ya wasanii wakubwa wakati bado akiwa msanii chipukizi.

"Kuna wasanii wakubwa unajitahidi kufanya kazi nao lakini hawaoni interest. Wakati mwingine unaweza ukaweka vesi yako kwa wimbo kisha ikatolewa kwa sababu bado hujapata kusikika. Lakini sasa siwezi kukataliwa mimi ni msanii mkubwa,"

Melody aliweka wazi kwamba kuna baadhi ya wasanii ambao ana washabikia sana nchini kenya, miongoni mwao;msanii Otile Brown,Jovial,Mejja,Msauti miongoni mwa wasanii wengine.

"Wasanii wa Kenya ambao nawashabikia sana ni,Jovial,Otile,Mejja,masauti na wengine wengi ambao nawapenda kwa ajili ya kazi ya nzuri."

Mwimbaji huyo wa kibao 'Sugar' alikiri kuwa mwanzoni alikabiliwa na changamoto kubwa ya kuwaaminisha watu kuwa anajua kuimba.

Alisema kuwa nyimbo za Kenya zinachezwa na kupendwa sana nchini Tanzania hasa jijini Dar es Salaam.

Wakati wa mahojiano hayo, mwanamuziki huyo kijana pia alifunguka kuhusu safari yake ya muziki kuanzia akiwa mwandishi wa nyimbo hadi kuimba nyimbo zake.