"China Square!" Manzi wa Kibera afunguka kuhusu asili ya makalio yake makubwa

Ni ya kujitafutia imagine, hii ni ya kujihustlia mwenyewe," alisema.

Muhtasari

•Manzi wa Kibera aliweka wazi kuwa sehemu hiyo ya mwili wake ni ghushi kwani ilifanyiwa kazi na wataalamu wa urembo.

•Mwanasosholaiti huyo lisema licha ya kutokamilisha masomo yake ameweza kupata shahada mbili katika masomo tofauti.

ndani ya studio za Radio Jambo
Manzi wa Kibera ndani ya studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Mwanasosholaiti mashuhuri Sharifa Sharon Wambui almaarufu Manzi wa Kibera amekiri kuwa makalio yake makubwa sio ya asili.

Akishiriki mahojiano na mtangazaji Massawe Japanni kwenye Radio Jambo siku ya Alhamisi, kipusa huyo aliweka wazi kuwa sehemu hiyo ya mwili wake ni ghushi kwani ilifanyiwa kazi na wataalamu wa urembo.

"Sio halisi, ni China Square. Sifichi! Kwa nini ning'ang'ane kuficha. Hakuna kitu ya kuficha," Manzi wa Kibera alisema.

Aliongeza, "Ni ya kujitafutia imagine, hii ni ya kujihustlia mwenyewe."

Alifichua kwamba alifanya majaribio mengi yaliyofeli kabla ya hatimaye kupata umbo wa makalio kamili ambao alihitaji.

Alisema kwa sasa anatumia unga ambao huwa anachanganya na maji na kunywa kila asubuhi na jioni ili kupata umbo lake.

"Imenichukua miezi kama nane kufikia hapa. Kuna shinikizo sana siku hizi, kuna shinikizo ya kukaa vizuri. Kuna shinikizo la kupata makalio kwa sababu wanaume wanataka vile," alisema Manzi wa Kibera.

Mwanasosholaiti huyo kutoka mtaa wa Kibera, jijini Nairobi pia aliweka wazi kuwa hana elimu kubwa licha ya kuwa maarufu.

Hata hivyo, alisema licha ya kutokamilisha masomo yake ya shule ya msingi ameweza kupata shahada mbili katika masomo tofauti.

"Nilisoma kidogo. Nadhani nilivukishwa shule ya chekechea nikasoma darasa la pili na la tatu. Shule ilikuwa inanichosha. Ilinichosha nikiwa katika darasa la pili la tatu hivi lakini niko na shahada," alisema.

Manzi wa Kibera ambaye alijizolea umaarufu miaka michache iliyopita alifichua kwamba, kando na kuwa na cheti ghushi cha shule ya msingi na cha shule ya upili, pia anamiliki shahada ghushi ya Ubunifu wa Usanifu na ya Rasilimali Watu.

"Ni kazi tu sijapata. Mnaninyima kazi na niko na digrii mbili?? Mnitafutie kazi," alisema.

Kidosho huyo aliweka wazi kuwa hana mpango wa kurejea shuleni kwani tayari ana mali za kumwezesha kujikimu kimaisha.