Mwalimu mkuu anawabebesha wanafunzi kuni za kuuza-Mwanamume asimulia

Muhtasari
  • Mwanamume allamika baada ya mwalimu mkuu kubebesha wanafunzi kuni
Teke Teke:Mbusi na Lion
Image: Studio

Siku chache baada ya shule kufunguliwa nchini kote na wanafunzi pamoja na wazazi kutabasamu kwa ajili ya kufunguliwa kwa shule baada ya wanafunzi kukaa nyumbani miezi kumi kwa ajili ya janga la corona.

Baada ya wanafunzi kurudi shule visa vya mauaji vimeripotiwa huku kwa upande mwingine walimu wakiwatuma wanafunzi pesa za kulipa mtihani wiki chache baada ya kurudi shuleni.

Hii leo katika kipindi cha Mbusi na Lion teketeke, katika radiojambo kitengo cha nyahunyo mwanamume mmoja alipiga simu na kueleza jinsi mwalimu mkuu anawatesa watoto kwa kubeba kuni.

 

"Mwalimu mkuu wa shule ambapo watoto wangu wanasoma anawatesa wanafunzi kwa kuwabebesha kuni, za kuuza na kisha anawatuma nyumbani wapeleke pesa ya mtihani shilingi miamoja

Watoto wangu ni wasichana mmoja yuko darasa la nne na la saba,jana walirudi nyumbani saa mbili usiku nilipowauliza waliniambia walikuwa wanabeba kuni wakipeleka kwa gari shuleni." Mwanamume huyo alisimulia

Mwanamume huyo alidai kwamba alipomuuliza mwwalimu mkuu alisema kwamba anawafunza watoo kazi.

Je maoni yako ni yapi kuhusu jamo hilo?