Kila wakati tukienda 'date' na mpenzi wangu huwa nalipa kila gharama ata nauli-Mwanamke afichua

Muhtasari
  • Mpenzi wangu amekuwa akinitegemea kwa kila kitu ata tukienda date

Ni nini haswa kama mwanamke umemfanyia mpenzi wako na kisha jambo hilo likakuudhi licha ya yako kuwa umempenda na roho yako yote.

Kuna baadhi ya wanaume watafanya jambo kimakusudi ili kuangalia kama unampenda, lakini kuna wale ambao ni wazembe wanataka wapenzi wao wafanye kila kitu.

Lakini swali langu ni je kwa nini umpeleke mpenzi wako kujivinjari kama mwanamume na huna pesa unamtegemea alipe kila kitu,si chakula,si burudani na hata kulipa nauli.

Kama wajua vyema huna pesa za kumpeleka mpenzi wako kuvinjari fichua mambo na umwambie kuwa mambo jinsi yalivyo.

Mwanamke mmoja aliichua yale amekuwa akimfanyia mpenzi wake katika kitengo cha Nyahunyo kwenye radiojambo.

"Chenye huwa na shangaa na mpenzi wangu ni kuwa kila wakati tunaenda date na yeye hagharamikii chochote, ni mimi nitalipa kila kitu hata nauli

Huwa akiitishwa nauli na makanga ananiangalia ili nitoe pesa nilipe, kuna wakati nilienda kukaa mbele na yeye nyumba makanga alipomuitisha pesa alinyoosha kidole vizuri na kuonyeshana kwenye nilikuwa nimekaa ili nilipe

Tumekuwa kwa uhusiano kwa miaka 4." Alieleza Mwanamke.

Je ina maana kuwa mpenzi wako wa kike hawezi gharamikia majukumu yeyote, na je kwanini wanaume wasijitolee na kugharamikia?

Mwanamume huyo ana makosa au la?