Mwanabodaboda mwezangu huwa anawabeba wateja kisha anawaibia-Mwanamume asema

Muhtasari
  • Mwanabodaboda mwezangu huwa anawabeba wateja kisha anawaibia
Radia Jambo presenters Lion and Mbusi
Radia Jambo presenters Lion and Mbusi

Wanabodaboda wamekuwa wakilaumiwa kwa kila mambo yote mabaya na wananchi hasa kuwatongoza watoto wa shule.

Mnamo siku ya JUmanne mwanamume mmoja alipiga simu kwenye radiojambo ili mwanabodaboda mwenzake atolewe makosa kwa tabia ambazo amekuwa akifanya.

"Kuna mwendesha bodaboda mwenzangu ambaye ametuharibia jina eneo hili, hii ni kwa sababu amekuwa akiwabeba wateja kisha anawapora

 

Huwa anaenda akifika mahali hamna watu anawaibia kisha anawaacha,huyo jamaa amekuwa akitenda kitendo hicho kwa muda."Alieleza Mwanamume huyo.

Je ni tabia zipi ambazo wanabodaboda hutenda na kuwaghadhabisha watu wengi, hasa wanawake.

Mwanamume huyo alisema kwamba hajaweza kufanyiwa ila tu amesikia malalamishi kutoka kwa wateja wao na wenzao.