Mwenye nyumba amekuwa akiambia wazazi wangu nikileta warembo kwa nyumba-Adai Mwanamume

Muhtasari
  • Mwanamume agadhabishwa na tabia hii ya mwenye nyumba

Katika kitengo cha nyahunyo ndani ya Radiojambo mwanamume mmoja alisimuia jinsi mwenye nyumba amekuwa akisema mambo ambayo anafanya kwa wazazi wake.

Alihitaji mwenye nyumba apigwe nyahuny ambapo mashabiki wa Radiojambo walipitisha anapaswa kupewa nyahunyo awache tabia hiyo.

"Niko chuo kikuu naishi katika nyumba ya kukodisha, kuna tabia ya mwenye nyumba ambayo imenikasirisha sana

 

Ndio sikatai nimekuja kusoma lakini pia kuna wakati wa kujivinjari na kufurahia, mwenye nyumba amekuwa akiwaambia wazazi wangu kwamba huwanaleta warembo kwangu

Yaani siwezi fanya kitu chochote  akiwa karibu kwa maana atafikisha ripoti chochote kile nimefanya

Nashindwa kazi yake ni kupokea pesa au ni kufikisha chote kile nimekuwa nikifanya," Alieleza.

Ndio kila kitu kina wakati wake, kama ni kuleta warembo kwa nyumba yako kwani unawabadilisha kila siku kama nguo?

Kuwa na mpenzi mmoja, japo kuwa wengi husema vunja mifupa hungali kijana, kwa hivyo mwanamume huyo anatimiza usemi huo.