Nyahunyo:Nikikosana na rafiki yangu huwa anamuacha mumewe tupigane-Mwanamke asema

Muhtasari
  • Mambo ya wanawake ni ngumu sana kwa wanaume kuelewa, haswa wanatka nini na wanachukia nini maishani mwao
  • Ni kauli ya  wanaume wengi kwamba baadhi ya wanawake hawaeleweki, kwani huwa na mdomo kaya
Mbusi na Lion

Mambo ya wanawake ni ngumu sana kwa wanaume kuelewa, haswa wanatka nini na wanachukia nini maishani mwao.

Ni kauli ya  wanaume wengi kwamba baadhi ya wanawake hawaeleweki, kwani huwa na mdomo kaya.

Hawakukosea waliposema wanawake wakikorofishana basi hamna mwanamume yeyote ambaye anapaswa kuingilia kwani hajui walianza ugomvi wao siku gani au lini.

 
 

Lakini kuna baadhi ya wanaume ambao wanapenda kuwatetea wanawake wao baada ya kuwa katika ugomvi na wanawake wenzao.

Katika kitengo cha nyahunyo, mashabiki wa radiojambo waliamua mwanamume mmoja apewe nyahunyo baada ya kuingilia vita ya mkewe na rafiki yake.

Huu hapa usimulizi wa mwanamke huyo.

"Nikikosana na rafiki yangu huwa anamuacha mume wake tunabishana, mumewe huwa anamwambia aende kwa nyumba apambane na mimi, hayo ni makosa makubwa kwa maana mwanamume huyo sio mwanamke

Hapaswi kuingilia mambo ya wanawake ovyp ovyo, mimi nataka apewe nyahunyo kwa maana huwa wananikosea sana kwa kuingilia mambo yetu," Alisema Mwanamke huyo.

Je mwanamume huyo alistahili kupewa nyahunyo au alikuwa na haki ya kumtetea mkewe?